UWEKEZAJI KWA VIJANA WA SEKONDARI UMEKUA UKILETA MANUFAA KATIKA SEKTA YA MICHEZO NCHINI
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa pili kulia)
akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufungua mashindano ya COPA UMISSETA
uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, wa kwanza
kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yussuph
Singo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya
CocaCola Eric Ongara na anayefuatia ni Rais wa Wakuu wa Shule za Sekondari
Tanzania (TAHOSSA) Bw.Vitalus Shija.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiongea na
wanafunzi wa shule za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kwa
mashindano ya COPA UMISSETA katika uwanja wa mpira wa Taifa.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia)
akisalimiana na washiriki wa michezo ya COPA UMISSETA inayoshirikisha shule za
Sekondari za Serikali na Binafsi iliyofunguliwa leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akipiga mpira
kuashiria kufungua mashindano ya michezo ya COPA UMISSETA inayoshirikisha shule
za Sekondari za Serikali na Binafsi leo Jijini Dar es Salaam.
Dhana ya kuwekeza
katika sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa shule za Sekondari imekua ikileta manufaa
makubwa kwa Taifa katika kuzalisha wachezaji mahiri ambao wamekua wakipeperusha
bendera ya Tanzania ndani na nje ya chini.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
alipokua akifungua michezo ya COPA UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari
za Serikali na Binafsi leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
“Nimefurahishwa na
juhudi zinazofanywa na Kampuni ya CocaCola katika kuhakikisha tunaimarisha
sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa kufanya hivyo
tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa kupata wanamichezo mahiri wa baadaye” amesema Waziri
Mwakyembe.
Aidha aliongeza kuwa Serikali
itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia vijana riziki pamoja na kuchangia katika
uchumi wa nchi.
Vilevile aliwataka walimu
kufuata ratiba za vipindi vya michezo kwa kuhamasisha michezo mashuleni ikiwemo
kuwapatia wanafunzi nafasi ya kujifunza na sio kuvitumia vipindi hivyo kwa
shughuli nyingine.
Hata hivyo Mhe.
Mwakyembe aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanawapatia watoto wao
nafasi ya kucheza na kujifunza michezo mbalimbali inayowajenga kimwili na
kiakili.
“Michezo inafaida
kubwa kwa afya ya binadamu ikiwemo kuimarisha
akili na mwili, kujenga ushirikiano na urafiki baina ya watu “ alisema Mhe. Mwakyembe.
Naye Mkurugenzi wa
Rasilimali watu wa Kampuni ya CocaCola Bw. Eric Ongara alisema kuwa Kampuni ya
CocaCola inaamini katika kuibua vipaji kuanzia ngazi ya chini ndio maana wamekua
wakidhamini mashindano hayo.
Pia aliongeza kuwa
Kampuni ya Coca-Cola itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa
michezo inazaa matunda na kufikia lengo lililokusudiwa la kuibua vipaji vya
michezo na kuviendeleza.
Michezo ya COPA
UMISSETA ilifunguliwa rasmi Mjini Dodoma
Aprili 28 mwaka huu ambapo kitaifa yanatarajiwa
kuanza Juni 6 hadi 15 mwaka huu katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu
Butimba Jijini Mwanza .
No comments