MAJERUHI 3 WA AJALI ILIYOTOKEA KARATU WAMESAFIRISHWA LEO KWENDA NCHINI MREKANI KWA MATIBU ZAIDI



Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akisalimiana na mmoja wa mtoto kabla ya safari,kushoto kwake ni mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu  akisalimiana na majeruhi hao
Mmoja wa majeruhi akiandaliwa tayari kubakizwa kwenye gari maalumu kuelekea kwenye ndege tayari kwa safari ya kuelekea nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi.
Mmoja wa majeruhi akipandishwa kwenye gari maalimu kwanjili ya kuingizwa kwenye ndege kwaajili ya kuanza safari ya kuelekea nchini Marekani kwaajili ya matibabu.
Gari maalumu lliliowabeba majeruhi hao na kuwasaidia ili waweze kuwaingiza kwenye ndege ya Samaritan.
Ndege hiyo ijulikanayo kama Samaritan Purse DC 8 N782SP imewasili jana May 13 ikiwa na Marubani wanne na Wahudumu wake 7  tayari kuwabeba Majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwenye matibabu.
dereva kufikia 34 
 Majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi la Lucky Vicent wakipakiwa kwenye Ndege ya Taasisi ya Samaritan's Purse ambao wamejitolea kuwahudumia kwa matibabu majeruhi hao kwa kuwasafirisha nchini Marekani kwa Matibabu zaidi huku majeruhi hao wakiongozana na wazazi wao, daktari mmoja na nesi mmoja kwa kila majeruhi
 Ndege ya Taasisi ya Samaritan's Purse ikiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mapema leo asubuhi tayari kwa kuruka mpaka Marekani kwaajili ya kuwapeleka majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky vicent iliyotokea wiki iliyopita na kupoteza watu 34 huko Karatu.
 Sehemu ya ndani ya Ndege ya Samaritan's Purse iliyowabeba majeruhi watatu wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ambao leo wamesafirishwa kuelekea nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi huku gharama za matibabu hayo yakitolewa na taasisi ya Sammaritan's Purse.
Baadhi ya wananchi, ndugu jamaa na wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha waliojitokeza kwaajili ya kuwasidikiza majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky Vicent iliyotokea wiki iliyopita huko Karatu Arusha Tanzania.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Zikiwa zimepita siku tisa (9) tangia kutokea kwa ajali iliyoleta simanzi kwa Taifa zima la Tanzania na Dunia kwa Ujumla, ajali hiyo ilihusisha basi dogo la Wanafunzi na kukatisha uhai wa wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1, huku ikiacha majeruhi 3 ambao  leo hii wamesafirishwa kuelekea nchini Marekani kwa matibabu zaidi.

Akizungumza katika kiwanja cha ndege cha KIA,mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemshukuru Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro , Syemm,Samaritans Purse pamoja na Wamarekani kwani watoto wetu wanaelekea huko na tunaamini watahudumiwa vizuri.

Majeruhi hao ambao ni Doreen Mshana (13), Sadia Ismael Awadhi (11) na Wilson Geofrey Tarimo (11) wameongoza na wazazi wao huku kila mmoja akiwa na usaidizi wa daktari mmoja na nesi mmoja kutoka hospitali ya Mount Meru Arusha.


"Kazi hii kubwa na Ngumu  ni kama tunaifikisha nusu ya safari leo,kazi kubwa ulikuwa kuwazika wale 35,kazi nyingine iliyokuwa Ngumu zaidi  ni ya kuhakikisha kuwa hawa majeruhi( 3) wanakwenda kupata matibabu nje ya nchi" alisema Gambo.

Kwa kushirikiana na Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kumewezesha kupatikana msaada wa kuwapeleka majeruhi wa ajali hiyo nchini Marekani kutibiwa bure na tayari ndege maalum yenye uwezo wa kufanya kazi kama Ambulance imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuwachukua majeruhi hao.

Gambo amesema kuwa tukio hilo siyo la kisiasa ,amewataka Watanzania na wananchi wa Arusha wasimkubali mtu yeyote kuwatoa kwenye lengo la msingi la kutoa huduma kwa watoto hao.

"Wakati sisi tunahangaika kuzika watu,tunahangaika kuwasafirisha kwenda kutibiwa,watu wengine wanatumia mitandao ya kijamii kutaka kupotosha malengo ya serikali na wadau wengine ,kuhakikisha kuwa wahusika wetu wanapata matibabu salama" alisisitiza Gambo.
Mmoja wa rubani wa ndege hiyo akiwa na Mbunge Lazaro Nyalandu kwenye uwanja wa Ndege KIA.

Ndege hiyo ijulikanayo kama Samaritan Purse DC 8 N782SP imewasili jana May 13 ikiwa na Marubani wanne na Wahudumu wake 7  tayari kuwabeba Majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwenye matibabu.

Rubani wa Ndege hiyo amewaambia Waandishi kwenye uwanja wa ndege Kilimanjaro (KIA) kwamba wataondoka leo May 14 na watasimama Cape Verde kuweka mafuta na kisha kuelekea Marekani moja kwa moja na wanatarajia kuingia jumatatu

Vero Ignatus   Blog inapenda kuwatakia safari njema ya matibabu yao Na Mungu akapate kuwaponya haraka ili kusudi wareje kuendelea na maandilizi ya mtihani wao wa Taifa wa Darasa la Saba.


No comments