SERIKALI YAANZISHA KIKAZI KAZI CHA KUDHIBITI UHALIFU WA JINAI KATIKA TASNIA YA MISITU NA WANYAMAPORI.
SERIKALI
imeanzisha kikosi kazi cha kudhibiti uhalifu wa kijinai katika tasnia misitu
na wanyamapori ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kupambana na
ujangili na biashara haramu ya wanyamapori na mazao ya misitu wa mwaka 2014-19.
Akiwasilisha hotuba
ya makadirio ya mapato na matumizi jana Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa
Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema kikosi kazi hicho
kinatumia teknolojia ya ndege maalum zisizo na rubani na mbwa maalum kwa ajili
ya kukabili ujangili na biashara haramu ya nyara za Serikali.
Anaongeza kuwa hadi
sasa Wizara iliendesha jumla ya siku-doria 349,102 ndani na nje ya maeneo
yaliyohifadhiwa na kuwezesha kukamatwa
kwa watuhumiwa 7,085 na meno ya tembo 129 na vipande vya meno 95 vyenye uzito
wa jumla ya kilo 810.03.
Profesa Maghembe
anaongeza kuwa Wizara yake pia ilifanikiwa
kukamata silaha za kivita 48, silaha za kiraia 150, risasi 1,058, magobore 406,
silaha za jadi 22,307,roda 120,538 pamoja na pikipiki 189, baiskeli 214, magari
20, ng’ombe 79,831 na samaki kilo 4,043.
“Kupitia doria hizo
jumla ya kesi 2,097 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali h nchini, jumla ya
kesi 802 zilikamilika ambapo kesi 262 zenye watuhumiwa 472 walifungwa jela ya
miezi 42,153” alisema Profesa Maghembe.
Akifafanua zaidi
Profesa Maghembe alisema kesi nyingine 43 zenye watuhumiwa 79 zilikamilika kwa wahusika
kuachiwa huru wakati kesi 276 zenye watuhumiwa 469 walilipa faini jumla ya Tsh.
Milioni 452 na kesi 966 bado zinaendelea.
Kuhusu mfuko wa
wanyamapori, Prof. Maghembe anasema katika mwaka 2016-17 mfuko umetumia Tsh
Bilioni 6.7 kuwezesha utekelezaji wa
kazi za kuhifadhi na miradi ya maendeleo zikiwemo doria na kukiwezesha kikosi
kazi maalum cha kupambana na ujangili.
Nuru Juma na Husna
Saidi
MAELEZO.
DAR ES SALAAM.
No comments