WAAJIRI WAPEWA SIKU 30 KUFIKISHA MICHANGO YA WATUMISHI WAO.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Dr.Ashatu Kijaji  akifungua mkutano mkuu wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF uliofanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa mfuko.Picha na Vero Ignatus Blog.
 
Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Daud Msangi akizungumza katika mkutano wa nane wa Wadau wa mfuko wa Mafao ya kustaafu wa GEPF ,,leo Jijini Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.
 
 Mwenyekiti wa bodi ya GEPF Joyce Shaidi akizungumza katika mkutano huo ambapo amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni "Hifadhi ya jamii kwa wote inawezekana katika uchumi wa viwanda"kauli mbiu hii imewekwa maksudi na kumuunga mkono Rais katika kujenga uchumi wa viwanda.Picha na Vero Ignatus Blog

 Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiongea katika mkutano huo ambapo alimuakilisha mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo .Picha na Vero Ignatus Blog
 
 
  Mtendaji mkuu Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akitoa neno la shukrani katika mkutano huo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kulia ni mtendaji mkuu wa UTT James WAshima akizungumza katika mkutano huo pembeni ni Mkurugenzi mkuu wa GEPF Daud Msangi
Wadau katika mkutano wakifatilia mada mbalimbali
 
Naibu waziri wa Fedha na Mipango  Dr.Ashatu Kijaji akizindua mpango wa gharama nafuu utakao wahudumia watu wote waliojiunga na mfuko huo.Picha na Vero Ignatus Blo.

 Picha ya pamoja.





NA, VERO IGNATUS-ARUSHA.

 Naibu waziri wa fedha na mipango Dkt Ashatu Kijaji ameziagiza bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii nchini katika kutekeleza majukumu yao kwa kufata sheria zilizopo kuwabana waajiri wa kampuni na taasisi mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo ya taifa na faida kwa wanachama na watakao kaidi wafikishwe mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa nane wa wadau na wanachama wa mfuko wa mafao wa GEPF Dkt Ashatu amesema sheria zipo wazi hivyo ni vyema viongozi wa mifuko kufata sheria ili kudhibiti uzembe unao endele kwa baadhi ya kampuni.

Dkt Ashatu ametoa siku 30 kwa waajiri hao ili kukamilisha michango ya wanachama kwani mpaka sasa serikali imeshakamilisha jukumu lake kwa maslahi ya jamii na wanachama wa mifuko ya hifadhi.

"Kama serikali ilikuwa inadaiwa na tayari imeshalipa shilingi bilioni 249 kiasi kilichosalia cha bilioni 35 kitakamilishwa ikifikapo 31juni 2017."alisema Kijaji 



Bi Joyce Shaidi ni mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa mafao wa GEPF akatumia fursa hiyo kupiga vita suala la matumizi ya madawa ya kulevya katika kuelekea Tanzania ya viwanda kwani nguvu kazi kubwa ya uzalishaji ni kwa vijana kwa maslahi ya taifa.
"Hadi sasa mfuko huu una jumla ya wanachama 1,14,462 pesa zilizopo kwenye mfuko kwa sasa ni shilingi Bilioni 428.09 tunatazamia ifikapo june 2017 mfuko utakuwa na bilioni 505,tunatarajia ifikapo 2020 mfuko utakuwa na trilioni 1"alisema mwenyekiti huyo.

Edward Nzota na Janeth Asajile ni miongoni mwa washiriki katika mkutano huo na mwanaeleza umuhimu wa kulipia michango ya mifuko ya hifadhi.

Mkutano huo unatarajiwa kuhitimishwa kesho ambapo pia naibu waziri wa fedha na mipango amekabidhi hundi ya shilingi bilioni moja kwa UTT kwa ajili ya mikopo ya shughuli za maendeleo nchini.


 
 



No comments