Watu wawili mwanamke na mwanaume wamekutwa wamefariki huku miili yao ukiwa imeteketea kwa moto,huku mwili mmoja ukiwa umefungwa kwa kamba mikononi.

Wananchi wakiwa nje ya nyumba ambapo tukio limetokea mtaa wa white rose kitongoji cha Elikyurei.Picha na Vero Ignatus Blog.
Nyumba ambayo alipokuwa anaishi marehemu Maureen Terewaeli Urio .
Chumba ambacho tukio limetokea (miili haipo imeshaondolewa na jeshi la polisi) picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus, Arusha.
Watu wawili , mwanaume na mwanamke wamekutwa wamekufa kwa kuchomwa na moto mitaa ya Whiterose, Kitongoji cha Elikyurei Kata ya Kiranyi Arusha Dc Majira ya saa tatu asubuhi Leo.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Onesphori Chami amesema kuwa wamemtambua marehemu mmoja wa kike Maureen Terevael Urio ambae alikuwa ni mpangaji katika nyumba hiyo inayomilikiwa na An'tujwa Msuya ambaye anaishi jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa mwanaume akiyekutwa amefariki hajaweza kutambulika mara moja,amesema kuwa miili hiyo imekutwa imechomwa na imefungwa kamba mikononi majira ya saa tatu asubuhi Leo
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Keranyi John Edward amesema kuwa taarifa ameipata Majira ya saa tatu asubuhi na haijafahamika chanzo cha vifo hivyo,kwani miili yote miwili imekutwa imechomwa juu ya godoro ,nyumba haijapata mdhara makubwa.
Blog hii ilimfatuta Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa wamemtambua marehemu mmoja ambaye ni Moureen Urio (32) mwanaume bado hajatambulika kutokana na mwili wake kuunguzwa vibaya na moto.
Mkumbo amesema kuwa baada ya kukutwa mwili umefungwa mikono inaonekana kuna waahalifu wametekeleza tukio hilo,jeshi la polisi Mkoani Arusha linaendelea na msako Wa kuwasaka wahalifu waliohusika na tukio hilo,miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitality ya Mount Meru.


No comments