RAIS DKT. MAGUFULI AMALIZA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI KILIMANJARO NA KUREJEA JIJINI DAR ES SALAAM.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadik katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadik wakati akielekea kupanda ndege katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.




URais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono na kuwashukuru viongozi mbalimbali wa Serikali, Kidini na Taasisi mbalimbali waliomsindikiza katika katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo. PICHA NA IKULU

















Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Mei 2017, amemaliza ziara ya siku Tatu mkoani Kilimanjaro, ambapo akiwa mkoani hapa pamoja na mambo mengine alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani - Mei Mosi.
 
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro - KIA, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Mecki Saidick.
.

No comments