RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA SHEREHE ZA MEI MOSI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitabasamu wakati Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa wanapita mbele yake kwa njia ya maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya.
Sehemu ya Wafanyakazi waliofika kwenye Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono wakati wa wimbo wa Mshikamano daima pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki, Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Saidik.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amenyanyua juu mikono mara baada ya kuimba wimbo wa Mshikamano Daima pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Saidik.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi M. Sadiki akitoa salamu za Mkoa kwenye Sikukuu hiyo ya Wafanyakazi Duniani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akitoa salamu katika Sikukuu ya Wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya akizungumza katika Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Azan Zungu akizungumza katika sherehe za mei mosi zilizofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro katika Chuo Kikuu cha Ushirika
Chama cha waalimu (CWT )wakipunga mikono Kwa fursha walipopita Kwa maandamano mbele ya jukwaa kuu .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakazi wawili wenye ulemavu mara baada ya kumaliza kuhutubia katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Wafanyakazi mbalimbali wakati akiondoka katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi mara baada ya kuhutubia katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani.
PICHA NA IKULU
Habari Na.Vero Ignatus ,Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekuwa mgeni rasmi katika sikukuu ya meimosi iliyofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro
Akizingumza na wafanyakazi katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi amesema kuwa mwakani serikali itatoa ajira katika sekta mbalimbali 52,000 hapo nyuma serikali ilishindwa kuajiri kwasababu kulikuwa na watumishi hewa,ambapo uhakiki unaendelea
Aidha amesema kuwa serikali imebaini wafanyakazi hewa 19,706 ambapo serikali ilikuwa inalipa shilingi Bilioni 19.48 ,ambapo kwa mwaka ilikuwa inapoteza jumla ya shilingi Bilioni 230 Kwa wafanyakazi ambao hawapo kazini
"Utashangaa kuona wafanyakazi hao hewa walikuwa wanalipwa mishahara,wanachukua likizo,mikopo,posho za safari,wanachukua hata mikopo kwenye mabenki wakati hawapo kabisa" alisema Rais
"Kuna baadhi ya wafanyakazi wamepunguza muda wao wa kuishi wengine ni wazee kabisa ila utashangaa hawataki kuondoka ili wawapishe wengine wafanye kazi kutokana na muda wao wa kustaafu kufika,nasema hao hawana tofauti na wenye vyeti feki,dawa yenu inachemka" alisema.
Amesema kuwa serikali imefanya uhakiki Wa vyeti feki 435,000,vyeti vya kugushi vimebainika ni 9932, Vyeti vyenye utata 1538,wenye vyeti vya taaluma bila kuwa na vyeti vya shule jumla yao ni 11,596 amewataka wenye vyeti feki kujiondoa mapema kabla 15 mei 2017 .
Rais amewataka wafanyakazi kuwa makini pale wanapotakiwa kuhamaa kituo kimoja cha kazi na kuhamia kituo kingine,wasihame hadi pale watakapopewa fedha zao za uhamishao.
"Usihame hadi pale utakapoona umepewa fedha zako za uhamisho ,wakishindwa kukulipa usiondoke endelea kukaa hapo endelea kufanya kazi." alisisitiza Rais.
Katika maadhimisho hayo ya mei Mosi amesema kuwa serikali ya awamu ya tano haina nia mbaya na hofu wafanyakazi amewaomba kuwa wavumilivu kwani madeni yao yatalipwa
"Serikali ya awamu ya tano haina nia mbaya na wafanyakazi madeni yenu yote yatalipwa ninachowaomba tuendelee kuvumiliana,muendelee kuutegemeza uchumi Wa nchi yetu,endeleeni kusimama katika umoja huu,mtangulizeni Mungu mbele Kwa kila jambo"
Ametoa wito kwa wazawa na wenyeji wa mkoa Wa Kilimanjaro waende kuwekeza katika mkoa huo kwani itawawezesha vijana wengi kupata ajira na uchumi wa Tanzania utaongezeka.
Amesema serikali ya awamu ya tano mwaka huu kufanya nyongeza ya mishahara ya kila mwaka ambayo itaambatana na kupandishwa madaraja ,nyongez hiyo zilikuwa imesimama kwaajili ya watumishi hewa, serikali itatoa ajira 52,000
.































No comments