GUGU HATARI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA NAIROBI (JKIA)

Na.Vero Ignatus .Arusha.
 
Gugu hatari la mmea unaodaiwa kupatikana katika maeneo machache hapa nchini  Tanzania unajulikana kama 'Gugu karoti' kwa kitaalamu 'Parthenium hysterophorus' umeonekana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.


Akinukuliwa habari hizi, mtaalamu mshauri wa Shirika la ECHO ukanda wa Afrika Mashariki ndugu Charles Bonaventure (Bonny), amesesema, “ni kweli kwamba gugu hili nimeliona uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nairobi asubuhi ya tarehe 30/04/2017,Ambapo amesema kuwa ni hatari kama jitihada ya kulitokomeza hazitachukuliwa kwa haraka litaendelea kuzagaa.
 
 " Changamoto kubwa nayoiona ni uelewa wa majani haya, hivyo elimu na uhamasishaji wa majani haya ni muhimu kutolewa kwa jamii” 

Aliendelea kusema gugu hili limezagaa njia nzima ya kutokea Nairobi mjini hadi sehemu za Kajiado na kwa upande wa Tanzania ameliona zaidi maeneo ya Ngaramtoni, Kwa Mrombo na Njiro. Pia limepamba barabara mpya inayojengwa inayotokea Sakina hadi Tengeru.

Inline image 1
Hivi karibuni mwandishi wa blog hii alikutana na mwananchi huyu ambaye hakupatikana jina lake mara moja amejipamba majani haya kwa ajili ya jambo alilokuwa analisheherekea  kama unavyoona katika picha.


 Majani ya gugu karoti ni hatari kwa afya za binadamu, wanyama na mimea.



No comments