WASHIRIKI WA KILLI MARATHON KUNUFAIKA NA TIGO 4G
| Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (kulia) akionyesha laini ya 4G internet zitakazotumika kwenye mashindano ya Killi Marathon yaliyodhaminiwa na Kampuni hiyo.Kushoto ni Meneja Mauzo wa Tigo Moses Busee.Picha na Ferdinand Shayo |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kampuni ya
Simu ya Tigo Imejipanga kuhakikisha kuwa huduma za mtandao wa 4G inapatikana
kipindi chote cha Mashindano ya riadha ya kimataifa ya Killi Marathon
yanayotarajia kufanyika Februari 26 mwaka huu katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi
wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata amesema kuwa kampuni hiyo itatua
mtandao wa kasi ya ajabu ya 4G katika
Mkoa wa Kilimanjaro na viunga vyake katika jitihada za kuhakikisha Washiriki wa
mbio hizo wanafurahia huduma zao.
Lugata
amesema kuwa kuboreshwa kwa huduma hizo kunatoa fursa kwa wafanyabiashara na
watalii katika mkoa wa Arusha kunufaika na fursa ya Mawasiliano inayotolewa na
Tigo.
“Wakazi wa
Moshi watakaokuja kwenye mashindano wataweza kutumia vizuri mitandao ya kijamii
kama facebook,watsap,skype na mingine mingi na kufurahia kutuma picha katika
mitandao” Alisema
Pia
Washiriki wa Mbio hizo wataweza kujipiga picha na kuzituma kwa watu
wanaowapenda kama njia mojawapo ya kuwajulisha watu kuhusu mashindano hayo.
Alisema kuwa
kampuni hiyo imejizatiti na kuongeza idadi ya minara ya simu ili kukuza na
kuboresha huduma za simu.
Lugata
amewataka Wakazi wa Kilimanjaro na mikoa yote ya Tanzania kujitokeza katika
Mashindano hayo ya kusisimua ndani na nje ya nchi.
No comments