Global Peace Foundation yamteua Idris wa Big Brother kuwa balozi wa Amani Tanzania
Taasisi
ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, imemteua mshindi wa Big
Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan, kuwa balozi wa amani kwa
vijana duniani.
Mkurugenzi
Mkazi wa GPF Tanzania, Martha Nghambi alisema kuwa wameamua kumtumia
Idris kutokana na mvuto wake kwa vijana na kutokana na hilo atafikisha
ujumbe kirahisi kwa vijana ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya
watu Tanzania.
Alisema
kuwa bado kuna changanoto nyingi za kudumisha amani duniani kwani mpaka
sasa kuna baadhi ya nchi zipo katika matatizo makubwa yaliyosababishwa
na uvunjifu wa amani.
Martha
alisema kuwa Idris ni mtu sahihi katika kampeni yao na wanaamini kuwa
kupitia yeye vijana na watu wengine watapata ujumbe wa kuhamaisha
kudumisha amani duniani.
“Kuna
baadhi ya nchi zina matatizo ya amani, waswahili wanasema, ukiona kwa
mwenzako kunawaka moto… kwako andaa maji, sisi tumeamua kuchukua
tahadhari mapema ili kulinda amani yetu,”
Kwa upande wake, Idris alifurahi sana kupewa nafasi hiyo ambayo ni kubwa sana katika maisha yake.
“Wamenithamini
na kuniona ninafaa katika kampeni hii, ni kweli, amani inatakiwa
kuanzia kwenye familia mpaka juu ambako wengi wanadhani vita tu ndiyo
inatakiwa kupigiwa kelele, vijana ndiyo nguvu kazi ya ya taifa na hivyo
tunatakiwa kuwa na mawazo yaliyopanuka ili kujipatia vipato na kuachana
na lawama kutokana na kukosa soko la ajira,” alisema Idris.
Alifafanua
kuwa kuwa balozi ni jukumu zito na atalitumikia ipasayo ili kufikia
malengo yaliyowekwa. “Amani ni kazi ya kila siku na ni muhimu, leo hii
wasanii wanaigiza na wanamuziki wanafanya kazi zao bila kuwa na woga,
hii yote inatokana na amani,” alisema.
Global
Peace Foundation ni shirika lisilo la kiserikali na lisilo tengeneza
faida lenye makao yake makuu, mjini Washington DC, Marekani. Shughuli
kubwa la shirika hili ni kuhamasisha amani duniani kupitia matawi yake
mbalimbali duniani.
Mbali
ya Tanzania, matawi mengine katika bara la Afrika ni Kenya, Uganda na
Nigeria. Kauli mbiu ya shirika hilo ni “We are all “One family under
God”(sisi wote ni familia moja kwa Mungu).
Kwa
sasa Global Peace Tanzania inaendesha kampeni ya kuhamsisha amani
kuanzia ngazi ya familia ijulikanyo kama “Vijana na Amani”. Kupitia
kampeni hii, GPF Tanzania inahamasisha amani kwa kutoa elimu katika
shule, vyuo na jamii kwa ujumla.
Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan (kulia), akipokea cheti cha utambulisho wa kuwa balozi wa Amani kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi.
Mkurugenzi
Mkazi wa Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, Martha
Nghambi (wa pili kushoto) na mshindi wa Big Brother Africa Hotshots
2014) Idris Sultan (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kutangazwa kuwa balozi wa amani kwa vijana Tanzania


No comments