SERIKALI ya Ujerumani imetoa Euro milioni 20.5 kwa ajili ya mradi wa kutekeleza Maendeleo mbalimbali ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Ngorongoro.
Aidha
fedha hizo zitawezesha uboreshaji wa miundo mbinu ya Ecosystem ya
Serengeti maarufu kwa jina la "Serengeti Ecosystem Devolopment and
Conservation Project (SEDCP)"
Akizungumza kwenye ofisi za TANAPA wakati wa kusaini mkataba wa mradi huo,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Serengeti Juma Keya alishukuru Ujerumani
kuwapatia fedha hizo zitakazofanikisha kukuwa kwa maendeleo ya wananchi
waliopo pembeni mwa Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro.
Amesema
baadhi ya shughuli zitakazotekelezwa na mradi huo ni pamoja na sekta ya
Elimu, Afya,maji safi,Nishati ya sola,mifugo na ujenzi wa miundo mbinu
ya barabara kwa Wilaya zote mbili.
"Mradi
huu utawezesha wananchi kufika katika masoko na kupata huduma zingine
za muhimu kwa kuwa na barabara safi, lakini kwenye Elimu kutakuwa na u
jenzi wa nyumba za waalimu, maabara na mabweni,"alisema
Pia
amesema kwenye sekta ya Afya wataboresha kwa kujenga Zahanati, nyumba
za Madaktari na Manesi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba,"alisema
Amewaomba wadau wa Ngorongoro kunisaidia mradi huo ufanikiwe badala ya kuingiza siasa.
Amesema
mkataba huo umesainiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),
Halmashauri ya Serengeti na wajumbe wa serikali ya Ujerumani.
Hata
hivyo wadau wa Halmashauri ya Ngorongoro wakiwakilishwa na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Ngorongori Methew Siloma hawakusaini mkataba huo kwa
madai mwaka wapate ufafanuzi wa mradi huo vizuri.
Naye
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti, Willium Mwakilema alishukuru
serikali ya Ujerumani na Taasisi zake kuamua kunisaidia Tanzania katika
maeneo hayo.
Aliomba kuepuka wadau kuingiza siasa katika Uhifadhi ili mradi usikwame.
No comments