Serikali kujenga Bandari ya kisasa Wete
Na Mwandishi wetu
Naibu
katibu mkuu UVCCM zanzibar Abdullighafari Idirisa Juma
amesema serikali ina mpango wa kujenga bandari mpya ya
kisasa wete ili kuinuwa shughuli za kiuchumi kwa wananchi.
Ameyasema
hayo huko bandarini Wete katika ziara yake ya kuangalia shughuli
mbali mbali za maendeleo pamoja na matawi ya ccm ikiwa
ni miongoni mwa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapindunzi..
Amesema
kukamilika kwa bandari ya wete kutatoa fursa kwa wananchi kisiwani
pemba kuendeleza shughuli zao za biashara kwa uhakika .
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wete,Rashid Hadidi Rashid amesema
shughuli za uchumi katika wilaya hiyo zinaimarika kutokana na
kuwepo kwa miundombinu ya uhakika ikiwemo maji safi na salama barabara
pamoja na umeme jambo ambalo linawafanya wananchi kujiimarisha
kiuchumi kwa miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
Nae Mkurugenzi wa bandari Pemba, Hamad Salim Hamad amesema tayari kumejitokeza mfanya biashara ambae anataka kuwekeza katika bandari hiyo
No comments