Afya ya Rais Mugabe Yazua Utata
Rais
wa Zimbabwe, Robert Mugabe, yuko nchini Singapore kwa ajili uchunguzi
wa afya yake, huku maofisa wa serikali wakikanusha taarifa za kiongozi
huyo kuzidiwa,
Kwa
mujibu wa gazeti la serikali la Sunday Mail Rais Mugabe aliondoka
nchini humo Ijumaa wiki iliyopita kuelekea nchini Singapore kwa matibabu
na kwamba kiongozi huyo anatarajiwa kurejea katikati ya wiki hii.
Safari
za rais Mugabe nchini Singapore zimeongezeka kwenye miaka ya hivi
karibuni ambapo mara ya mwisho kuwa nchini humo ilikuwa ni mwezi Mei
ambapo pia alisafiri kwa sababu za kimatibabu na mwaka 2011 na 2014
alifanyiwa upasuaji wa jicho.
Afya
ya Rais Mugabe imeendelea kuzua mijadala nchini mwake ambapo mwezi
Machi mwaka huu mamlaka nchini humo ziliwakamata waandishi wa habari
wawili walioandika kuwa afya ya kiongozi huyo imezorota.
Licha
ya umri alionao, chama chake cha ZANU-PF mwaka jana kilimteua
kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao, huku
kukiripotiwa mgawanyiko ndani ya chama hicho.

No comments