Tukuwani Riime’ jukwaa la wanaume kuipigania jamii kiafya Afrika Kusini

‘Tukuwani Riime’ jukwaa la wanaume kuipigania jamii kiafya Afrika Kusini

UNAIDS
Photo: UNAIDS
 
Kuelekea ya Siku ya Kimataifa ya UKIMWI itakayoadhimishwa Jumapili hii, ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI  (UNAIDS) iliyotolewa juzi Jumatano imeeleza kuwa dunia inaweza kufikia lengo lililokubaliwa la kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 lakini kwa sharti kwamba viongozi ni lazima walinde haki za binadamu za kila mtu anayeishi na Virusi Vya UKIMWI, VVU au aliyeko hatarini kuambukizwa. 

Mmoja wa mifano mizuri ya juhudi hizo ni wa Afrika Kusini unaofahamika kama “Takuwani Riime”.“Takuwani Riime” ni neno kutoka lugha ya kibantu ya Tshivenda ikimaanisha “Tusimame pamoja” wito wa wazi kwa wanaume kuchukua hatua katika ngazi zote za kijamii kuendeleza usalama wa jamii na afya ya watu nchini Afrika Kusini.
 
UNAIDS inasema theluthi mbili ya watu wote wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI, VVU duniani wanapatikana Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ndio maana Jukwaa la Wanaume (Takuwani Riime) linalenga kurekebisha hili na kuwafanya wanaume na wavulana na jamii kujua hali zao za VVU.
 
Hiyo ni sauti ya Charles Mphephu mwanzilishi wa Jukwaa la Wanaume akipita mtaani katika kitongoji duni cha Alexandra jijini Johannesburg. Anasema, “Wanajamii mnakaribishwa kuja, kupima VVU, TB na huduma za afya leo. Inaanza saa 10 hadi 12. Unakaribishwa zaidi kuja na mwenzako.”
 
Na kweli, vibanda vimewekwa mtaani watu wanakuja kupima VVU. Aliyeambukizwa anaanzishiwa dawa, asiyemabukizwa anapewa ushauri wa kujikinga. Na hivyo ndio UNAIDS inavyotaka.

Chanzo UN

No comments