Mfumo wa M-Mama unavyosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto
Mfumo wa M-Mama unavyosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto
Waandishi wa habari na maafisa habari wa mikoa ya Manyara Singida na Dodoma, wametakiwa kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa mfumo wa M- Mama ambao utasaidia kuokoa Maisha ya wanawake na watoto wachanga.
Akizungumza katika semina iliyofanyika jijini Dodoma ambayo imewakutanisha waandishi wa habari wa Mikoa hiyo,
katibu tawala msaidizi afya ustawi wa jamii Thomas Rutachunzibwa amesema serikali imehakikisha Vifo vya mama na mtoto vinapungua kwa kutumia mfumo wa M- Mama ambao unasaidia kutatua changamoto ya usafiri pale kunapotokea dharura.
Rutachunzibwa amewataka wananchi kupiga Bure namba 115 Ili waletewe usafiri na kupelekwa katika kituo Cha afya Bure kunapotokea changamoto ya dharura Kwa mama mjamzito, mtoto mchanga wa kuanzia siku 0 hadi 28 pamoja na mama aliyejifungua mwenye chini ya siku 48.
Amesema lengo la kuanzishwa mfumo huo ni baada ya kuwepo Kwa changamoto ya usafiri Kwa makundi hayo hali ilivyokuwa ikipelekea kuwepo Kwa Vifo vingi, hivyo mfumo huu unaokoa maisha kwani unawasaidia kuwawaisha walengwa kwenye vituo vya afya .
Kwa upande wake mratibu wa mfuko wa M- Mama Dodoma kupitia shirika la Pathfinder International Abdallah Issa ambao walikuwa wadhamini wa mafunzo hayo amesema mfumo huu umeanza kutumika nchi nzima Ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Afisa afya mkoa wa Manyara Suten Mwabulambo, amesema makundi ya wanawake wajawazito na watoto ni makundi ambayo yanaambukizwa magonjwa ya mlipuko Kwa haraka hivyo serikali imefanya jitihada za kuokoa maisha ya makundi hayo Kwa kuwasogezea karibu huduma za afya.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wamesema elimu ambayo wameipata wataelimisha umma kupitia vyombo vyao vya habari juu ya faida za mfumo huo wa M- Mama na namna unavyofanya kazi.
Mratibu wa M-Mama kitaifa Meshack Mollel amesema kwa kushirikiana na shirika la pathfinder wameajiri madereva zaidi ya 4000 Katika mfumo usiokuwa rasmi ili kuwasaidia wanawake na watoto.


No comments