Dkt. Awezaye : Waafrika hata siri hatuna sababu ya lugha za kigeni, lazima tuwe na lugha yetu:

Waafrika hata siri hatuna sababu ya lugha za kigeni, lazima tuwe na lugha yetu: Dkt. Awezaye
Dkt. Philip Awezaye mhadhiri wa chuo kikuu cha KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini.
Dkt. Philip Awezaye mhadhiri wa chuo kikuu cha KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini.

Na Flora Nducha - Havana, Cuba

Huko Havana Cuba Kongamano la kimataifa la Kiswahili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki ambapo wadau kutoka nchi mbalimbali kuanzia barani Ulaya, Marekani kaskazini na Kusini, Asia na wenyeji Afrika walikutana na kujadili jinsi ya kukuza lugha ya Kiswahili duniani sanjari na kutekeleza malengo ya Umoja wa Mataifa kama kutumia Kiswahili kudumisha amani na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo ni mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha KwaZulu Natal ambaye ni raia kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC,

Akizungumza na Flora Nducha wa idhaa hii Dkt. Philp Awezaye amesema kuna haja kubwa ya kuhakikisha Waafrika  wanakuwa na lugha moja  watakayojivunia kuwa ni lugha yao pekee na yenye asili ya Afrika isiyo ya kigeni.

Washiriki katika Kongamano la kimataifa la Kiswahili leo limeng’oa nanga jijini Havana Cuba.
Washiriki katika Kongamano la kimataifa la Kiswahili leo limeng’oa nanga jijini Havana Cuba.

Je ulijifunza vipi Kiswahili?

Dkt. Awezaye amesema upande wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kideokrasia ya Congo DRC, Kiswahili kinapendwa na kuzungumza na watu wengi ingawa kinachanganywa sana la lugha za asili za eneo hilo au hata Kifaransa lugha moja ya lugha za taifa hilo.

Amesema “Tunaongea Kiswahili lakini si sanifu nah apo ndipo nilipopata msingi wa lugha ya Kiswahili.”

Ameongeza kuwa kwa sasa zaidi ya miaka 25 anaishi nchini Affrika ya Kusini ambako alipata elimu yake ya sekondari na chuo kikuu.

Kwa mujibu wa Dkt. Awezaye kupenda kwake Kiswahili “Ni kutokana na kujua kwamba siwezi kuendelea kutumia lugha za wazungu, Waafrika tunatakiwa kuwa na lugha yetu kwani hatuna siri hata tukitaka kuteta basi tunatumia lugha za kigeni.”

Amesisitiza kuwa hii sio kama hatuwapendi wageni la hasha “Lakini tunatakikana tuwe na lugha yetu ambayo tutatumia kama Waafrika.”

Ametaja sbabu zingine kuwa ni Kiswahili sasa kimekuwa lugha rasmi kwenye Muungano wa Afrika na kuna nchi nyingi zinazotumia lugha hiyo na kukichagiza Kiswahili ili watu wote wa Afrika waweze kukitumia kama lugha yao.

Dkt. Philip Awezaye (kulia), Mhadhiri wa chuo kikuu cha KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini akiwa na Flora Nducha huko Havana Cuba.
Dkt. Philip Awezaye (kulia), Mhadhiri wa chuo kikuu cha KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini akiwa na Flora Nducha huko Havana Cuba.

Je chuo cha KwaZulu Natal kinafundisha Kiswahili?

Ametanabaisha kwamba ndio kwanza waanza kuikumbatia lugha hiyo  kwa kasi kubwa.

Amesema “Tumeanza sasa hivi kufundisha Kiswahili , tumeweka mikakati , tumeweka fedha na nimekuuja na mkuu  wa Idara za lugha za Kiafrika profesa Zulu kwa sababu ytuna lugha zingine za Kiafrika , tuna pia Kizulu na lugha zingne za Aafrika Kusini.”

Ameongeza kuwa “Sasa tumeamua kuwa Kiswahili kiwe hapo na tumewek maandalizi kweli sasa tunanunua vitabu, tunatafuta kuajiri waalimu na kuangaia jinsi hgani tunaweza kuchagiza wanafunzi wetu kujifunza lugha hii ijijekuwa tu wanachukua lugha zingine kama Kifaransa au Kijerumani au lugha zingine, kwani tunataka kukiinua kabisa Kiswahili.”

Wanafunzi wa Kwaulu Natal wamekipokeaje Kiswahili?

Kwa mujibu wa Dkt. Aweezaye wanafunzi wa chuo kikuu cha KwaZulu Natal wako tayari kuanza safari ya kujifunza lugha mpya.

Pia amesema “Serikai ya Afrika ya Kusini sas hivi wameamuwa kuwa Kiswahili kiffunfishwe katika ngazizote za elimu kuanzia shule za msingi.”

Na kwa hivyo amesema “Sisi kama chuo Kikuu tumepewa hilo jukumu la kuanza kuwafunza wale ambao watakuwa waalimu, ambao watatumwa sasa kwenye hizo shule za msingi kufundisha ili Watoto wakikuwa watakuwa na lugha zao, kwa mil ana desturi.”

Ili kufanikisha hilo amesema  ndio maana wameiomba serikali ya Taanzania kuwashika mkono kwa sababu Watoto watajifunza lug ana mila za utamaduni wa Mswahili na Tanzania ndio chimbuko la lugha hiyo.

Ameongeza kuwa “Hii itakuwa vizuri kwa sababu sasa tutakuwa hatuwafundishi Watoto tu lugha na utamaduni wa kigeni bali watajifunza utamaduni wa Kiafrika na Kiswahili sasa huu ndio muda wake, kwani tukilenga mbele miaka kama 20 ijayo basi nasi tuwe na lugha yetu ambayo tunaweza tukaitumia tuongee kama Waafrika.”

Washiriki wa Kongamano la kimataifa la Kiswahili lililofanyika huko Havana Cuba.
UN News/Flora Nducha
 
Washiriki wa Kongamano la kimataifa la Kiswahili lililofanyika huko Havana Cuba.

Na Congo DRC utokako wamekibeba vipi Kiswahili?

Kuhusu Kiswahili nchini Jamhutri ya Kidemokrasia ya Congo DRC amesema lazima ikumbukwe kuwa Kiswahili kinapendwa sana lakini kimechanganywa sana.

Hata hivyo amesema “Lugha ambazo zinakubaliwa kama lugha za Taifa Kiswahili pia kimo na unaruhusiwa kuongea hata bungeni kwa Kiswahili.”

Hata hivyo amesema kutokana na changamoto “Kuna hitaji hapo la kuwa na waalimu ambao watafundisha hicho Kiswahili sanifu ambacho kitakuwa kwa watu wote, lakini pia kukubaliana na hizo tofauti za lugha  na hasa sasa ninafanya utafiti kwa ajili ya hizo tofauti na tunalinganisha na lugha zingine kama Kizulu huko Afrika Kusini.”

Pia amesema wanaangalia ni kwa nini kuna utofauti wa lugha hasa Congo na je watu wa Congoa wanaweza kusikilizana na watu wa sehemu zingine kama Kenya au Tanzania.

Pia amesema amebaini kwamba tofauti hiyo ya uzungumzaji waKiswahili iipo sehemu nyingi sio DRCc pekee.

“Nilikwenda Nairobi na nikabaini kwamba hata wao wanachanganya sana Kiswahili na kizungu au Kiingereza”

Hivyo ammesema itasaidia sana kwa kuwa Tanzania inazo idara ambazo zinaweza kufundisha Kiswahili fasaha ili kuzisaidia nan chi zingine kukumbbatia Kiswahili sanufu.

Nini wito wako kuhusu Kiswahili?

Dkt. Awezye amehitimisha kwamba “Kiswahili tunakipenda ni lugha tukufu lugha ambayo leo kwa Mawazo yangu ni kipaji mungu ametupatia.”

Lakini akaenda mbali zaidi na kusema “Kwa utafiti Kiswahili ndio lugha ambayo Waafrika wengi wanaizungumza. Watanzania wana bahati kuwa ni lugha mama yao`lakini ni lugha yetu sisi wote.”

Amemalizia kwa kusema kwamba kuna changamoto nyingi “Lakini ni wakati tuziombe serikali zetu zije Pamoja kuendeleza Kiswahili n ahata Umoja wa Mataifa tutawaunga mkono pia kama watafiti nanyi mtuungge mkono ili wanafunzi wetu waje huko kujifunza zaidi nanyi mje huku hilo ndilo ombi langu.”


No comments