SAUTI ZA WANANCHI; MIEZI SITA YA UONGOZI WA MHE. PAUL MAKONDA.
Alipofika Arusha mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na baadae kukabidhiwa Ofisi tayari kwa kuanza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa mkoa Mhe. Paul Christian Makonda aliahidi kuhakikisha kuwa kila Mwananchi wa Arusha ananufaika na nafasi yake,ili kuacha alama na maana chanya kwa maisha ya kila mwananchi wa mkoa huu wa Kaskazini mwa Tanzania.
Mambo sita aliyoyasema kama kipaumbele mnamo mchana wa Jumatatu ya Aprili 08, 2024 ilikuwa ni pamoja na kusimamia haki, kukuza uwajibikaji, kusisimua utalii na uchumi wa Arusha, kuimarisha na kukuza ulinzi na usalama wa Mkoa pamoja na kuwa mtatuzi wa kero na changamoto za wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha.
Leo Novemba 17, 2024 Mhe. Makonda anafanya mkutano na wanahabari kueleza tathimini na mafanikio ya Miezi yake sita kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, zoezi ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa Simba uliopo kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC Jijini Arusha.
No comments