SERIKALI KUFUNGA CAMERA OFISI ZOTE ZA SERIKALI NA UMMA KUDHIBITI VITENDO VIOVU.
SERIKALI KUFUNGA CAMERA OFISI ZOTE ZA SERIKALI NA UMMA KUDHIBITI VITENDO VIOVU.
Serikali ya Equatorial Guinea imesema hivi karibuni itafunga camera maalum za ulinzi kwenye Ofisi zote za Serikali ili kudhibiti vitendo viovu vya uvunjifu wa maadili vinavyofanywa kwenye Ofisi hizo ikiwa ni uamuzi ambao umekuja kufuatia kashfa ya ngono inayomuhusisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha Nchini humo, Baltasar Engonga ambaye amejirekodi akifanya mapenzi na Wanawake zaidi ya 400 Ofisini kwake na nyumbani.Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue amesema hayo baada ya kufanya kikao na Viongozi wa Mamlaka za Serikali kujadili kashfa ya video hizo za ngono ambapo amesisitiza hawatovumilia vitendo vinavyochafua taswira ya Uongozi na Serikali ya Nchi hiyo.Engonga ambaye ni Baba wa Familia ya Watoto sita, tayari amekamatwa kwa kosa la kujirekodi akiwa anafanya mapenzi na Wanawake hao ambao wengine ni Wake za Watu


No comments