United NationsHabari za UNAudio and SubscriptionKabrasha la SautiSajili Hatua zisipochukuliwa sasa watu bilioni wataishi 3 bila huduma za vyoo ifikapo 2030: UNChelsea Johannes (kulia) akifafanua jinsi chombo cha choo chao cha kibunifu cha Saniwise kinavyofanya kazi.© UNICEF/Paul Kidero Chelsea Johannes (kulia) akifafanua jinsi chombo cha choo chao cha kibunifu cha Saniwise kinavyofanya kazi.19 Novemba 2024 Tabianchi na mazingiraHii leo ni siku ya choo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema licha ya choo kuwa ni msingi wa kusongesha afya ya binadamu na kusaidia watoto wa kike na wanawake kuishi maisha ya utu, bado wakazi wengi wa dunia hususan kwenye mizozo na majanga wanaishi bila huduma hiyo ya msingi.Kupitia ujumbbe wake wa siku hii Guterres “Familia nyingi za kibinadamu zinaishi bila haki hii ya msingi ya kibinadamu. Kwa kiwango cha sasa, watu bilioni 3 bado wataishi bila huduma za usafi zinazosimamiwa kwa usalama ifikapo 2030.”Kaulimbiuy a Siku ya choo duniani mwaka huu 2024 kwa mujibu wa shirikika la Umoja wa Mataifa la masuala yam aji au UN Water ni “Usafi wa Mazingira kwa ajili ya Amani”, ikiangazia jukumu muhimu la vyoo salama na mifumo ya vyoo katika kujenga ulimwengu wa haki, afya na amani zaidi.Pia siku hii ya Choo Duniani ya mwaka huu inaangazia vitishio ya usafi wa mazingira vinayotokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi, majanga na kupuuzwa.Nini kifanyikeKwa mantiki hiyo ametaka serikali kuunga mkono Mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji na Huduma za kujisafi kulinda huduma za choo hata nyakati za mizozo na hali mbaya za hewa.Guterres amesisitiza kuwa “Ni lazima tufanye kazi kupanua wigo wa msaada kwa nchi zinazoendelea kupitia ufadhili na teknolojia ili kujenga na kudumisha mifumo hii inayoendeleza maisha.”Pia amesitaka pande zote kwenye mizozo lazima ziache kulenga miundombinu ya vyoo na maji.Amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa “Tusiache juhudi zozote za kutimiza ahadi yetu ya maji na usafi wa mazingira kwa wote, na kuhakikisha kwamba kila mtu duniani anaweza kutambua haki hii ya msingi.”Huduma za vyoo na tabianchiMaadhimisho ya mwaka huu yameenda sanjari na matukio kwenye Umoja wa Maataifa ambayo yanatumika kuanzisha majadiliano thabiti na mipango ya utetezi kuhusu usafi wa mazingira wenye mnepo dhidi ya mbadiliko ya tabianchi, na kuhamasisha Nchi Wanachama chini ya Mkakati wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Maji na Usafi wa Mazingira.Malengo ya hafla hiyo ni Pamoja na• Kujenga ufahamu juu ya usafi wa mazingira wenye mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kama hitaji la maisha ya amani na yenye heshima.• Kutoa msukumo wa msaada endelevu wa kisiasa na kifedha ili kuharakisha maendeleo katika usimamizi salama na mnepo wa usafi wa mazingira kuelekea kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu namba 6.2.• Kutambua njia za kuendeleza usafi wa mazingira ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Hatua zisipochukuliwa sasa watu bilioni wataishi 3 bila huduma za vyoo ifikapo 2030: UN
Chelsea Johannes (kulia) akifafanua jinsi chombo cha choo chao cha kibunifu cha Saniwise kinavyofanya kazi.
Chelsea Johannes (kulia) akifafanua jinsi chombo cha choo chao cha kibunifu cha Saniwise kinavyofanya kazi.

Novemba  19 ni siku ya choo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema licha ya choo kuwa ni msingi wa kusongesha afya ya binadamu na kusaidia watoto wa kike na wanawake kuishi maisha ya utu, bado wakazi wengi wa dunia hususan kwenye mizozo na majanga wanaishi bila huduma hiyo ya msingi.

Kupitia ujumbbe wake wa siku hii Guterres “Familia nyingi za kibinadamu zinaishi bila haki hii ya msingi ya kibinadamu. Kwa kiwango cha sasa, watu bilioni 3 bado wataishi bila huduma za usafi zinazosimamiwa kwa usalama ifikapo 2030.”

Kaulimbiuy a Siku ya choo duniani mwaka huu 2024 kwa mujibu wa shirikika la Umoja wa Mataifa la masuala yam aji au UN Water ni “Usafi wa Mazingira kwa ajili ya Amani”, ikiangazia jukumu muhimu la vyoo salama na mifumo ya vyoo katika kujenga ulimwengu wa haki, afya na amani zaidi.

Pia siku hii ya Choo Duniani ya mwaka huu inaangazia vitishio ya usafi wa mazingira vinayotokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi, majanga na kupuuzwa.

Nini kifanyike

Kwa mantiki hiyo ametaka serikali kuunga mkono Mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji na Huduma za kujisafi kulinda huduma za choo hata nyakati za mizozo na hali mbaya za hewa.

Guterres amesisitiza kuwa “Ni lazima tufanye kazi kupanua wigo wa msaada kwa nchi zinazoendelea kupitia ufadhili na teknolojia ili kujenga na kudumisha mifumo hii inayoendeleza maisha.”

Pia amesitaka pande zote kwenye mizozo lazima ziache kulenga miundombinu ya vyoo na maji.

Amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa “Tusiache juhudi zozote za kutimiza ahadi yetu ya maji na usafi wa mazingira kwa wote, na kuhakikisha kwamba kila mtu duniani anaweza kutambua haki hii ya msingi.”

Huduma za vyoo na tabianchi

Maadhimisho ya mwaka huu yameenda sanjari na matukio kwenye Umoja wa Maataifa ambayo yanatumika kuanzisha majadiliano thabiti na mipango ya utetezi kuhusu usafi wa mazingira wenye mnepo dhidi ya mbadiliko ya tabianchi, na kuhamasisha Nchi Wanachama chini ya Mkakati wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Maji na Usafi wa Mazingira.

Malengo ya hafla hiyo ni Pamoja na

• Kujenga ufahamu juu ya usafi wa mazingira wenye mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kama hitaji la maisha ya amani na yenye heshima.

• Kutoa msukumo wa msaada endelevu wa kisiasa na kifedha ili kuharakisha maendeleo katika usimamizi salama na mnepo wa usafi wa mazingira kuelekea kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu namba 6.2.

• Kutambua njia za kuendeleza usafi wa mazingira ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo Un

No comments