SIMANZI SIMANZI ,WANAFUNZI WANAFUNZI 33 WALIMU 2 NA DEREVA WAFARIKI KATIKA AJALI ..KARATU MKOANI ARUSHA


Basi la shule ya Lucky Vincent likiwa korongoni

Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, , Karatu mkoani Arusha.

Mkasa huo umetokea takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ,takriban kilomita 150 kutoka mji wa Arusha.

Wanafunzi hao walikuwa wamesalia na kilomita 5 ili kufika sehemu waliokuwa wakielekea.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amesema kuwa wanafunzi 33 wakiwemo walimu 2 pamoja na Dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo.

Kamanda Mkumbo  amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa tatu asubuhi wakati mvua inanyesha ambapo mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.

Amesema kuwa baada ya ajali hiyo miili yote 36 imepelekwa katika hospital ya Lutheran Karatu kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuipeleka Mount Meru Arusha kwa ajili ya ndugu zao kuitambua na taratibu za mazishi ziendelee ambapo uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia amewasihi wazazi pamoja na wana Arusha kuwa wavumilivu kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba mzito uliotokea katika Jiji la Arusha

Naye Mwalimu wa shule ya msingi Luck vicent ambaye ndiye mlezi wa wanafunzi hao Bwana Efrem Jackson amesema kuwa wanafunzi  hao walikuwa wanaenda English Medium Junior Schools  Karatu kwa ajili ya ujirani mwema na shule ya msingi ya Tumaini iliyoko Karatu kwa ajili ya masuala ya kimasomo.

Jumla ya watu waliokuwemo Ndani ya Gari hilo ni 38 waliopoteza maisha ni 36 wawili  ni majeruhi.

Amesema kwamba dereva alidaiwa kutoijua barabara hiyo hivyobasi alikosa mweleko na kuteleza kando ya barabara kabla ya kutumbukia korongoni katika mto Malera.


Harakati za uokozi zikiendelea


Wananchi pamoja na wazazi wakiwa wamekusanyika katika shuleni hapo

Aidha maiti zimehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru.

Mkuu wa wilaya ya Arusha , Gabriel Daqqaro  amewataka wananchi kuwa watulivu kutokana na tukio hilo baya, na kwamba serikali itatoa taarifa baadaye kuhusiana na msiba huo.

No comments