MMILIKI WA SHULE YA LUCKY VICENT APANDISHWA KIZIMBANI



Na.Vero Ignatus.Arusha

Mahakama ya hakimu mkazi Mkoani  Arusha imempamdisha kizimbani mmiliki wa shule ya Lucky Vincent bwana Inocent Simon Moshi Pamoja na makamu mkuu wa shule  bw.Longino Vicent Mkana na kusomewa mashtaka matano.

Mahakama hiyo imewafungulia kesi namba 77 ya usalama barabarani akisoma makosa hayo mbele ya hakimu kazi Desidery Kamugisha,Mwendesha mashtaka  Rose Sule ameiambia mahakama Innocent Simon Moshi anakabiliwa na makosa (4) kosa la (1) kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, mnamo tarehe 6mei 2017 akiwa mmiliki wa gari T.871 BSY Toyota Rosa alibeba abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji .

Aidha amesema kuwa kosa la pili ni kuruhusu gari kuendeshwa barabarani bila kuwa na Bima,kushindwa kuingia mkataba wa ajira na dereva wake Dismas Joseph Gasper(aliyefariki ),kubeba abiria kwenye gari na kuzidisha wengine 13.

Makamu mkuu wa shule anakabiliwa na kosa (1) yeye kama muandaaji wa safari alishindwa kutimiza majukumu yake .

Aidha watuhumiwa wote wawili wamekana mashtaka hayo,wameachiwa kwa bondi ya dhamana ya shilingi Milioni 15 kila mmoja huku wakitakiwa kutokusafiri nje ya mkoa na wawasilishe hati zao za kusafiria , ambapo  kesi hiyo  imeahirishwa na inatazamiwa kusikilizwa tena tarehe 8/06/2017.

Ikumbukwe kuwa ajali hii iliyosababisha vifo vya wanafunzi 33 walimu 2 na dereva 1 ilisababishwa na gari aina ya T 871 BYS Toyota  rosa kuacha njia na kudumbukia korongoni ,ajali hiyo ilitokea siku ya Jumamosi 6 Mei 2017 majira ya saa tatu asubuhi katika mteremko wa mlima Marera kata ya Rhotia, wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

No comments