Simbachawene Wakaguzi wandani kuweni makini.
![]() |
| Waziri George Simbachawene akizungumza na wakaguzi wa ndani katika mkutano unaoendelea kwa siku tatu katika kituo cha kimataifa cha mikutano (AICC)Katika ukumbi wa Simba. |
![]() |
| Waziri Simbachawene akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,aliyepo pembeni yake ni Mkuu wa wakaguzi wa ndani Mohamed Mtonga. |
![]() |
| Rais wa wakaguzi wa ndani Richard Magongo akizungumza na wakaguzi katika mkutano wa siku tatu ulioanza leo katika kituo cha kimataifa cha mikutano( AICC) katika ukumbi wa Simba. |
![]() |
| Waziri Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na wakaguzi wandani nchini Tanzania. |
.Na. Vero Ignatus Arusha.
Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tawala za serekali za mitaa na TAMISEMI George Simbachawene amewataka wakaguzi wa ndani katika halimashauri hapa nchini kuhakiksha wanasimamia kwa umakini mapato ya halimashauri ili kuchochea chachu ya maendeleo.
Waziri Simbachaweni ameyasema hayo leo hii kituo cha kimataifa cha mikutano (AICC)katika ukumbi wa Simba katika mkutano wa siku tatu ulioanza leo katika wa mkutano wa 10 wa wakaguzi wa ndani ambao uilofanyika jijini hapa ikiwa na lengo la wakaguzi hao wa ndani kuangalia njia muafaka za kukubiliana na changamoto wanazokubiliana nazo.
Amesema kuwa wakaguzi wa ndani katika halimashauri zetu ni watu muhimu sana katika kuangalia hali ya miradi inayoendeshwa na halmashauri kwa maana miradi mingi inafanywa na halmashauri zetu na hivyo kupelekea kuingiziwa pesa nyingi.
Aidha waziri huyo wa TAMISEMI amesema kuwa kwa sasa wameagiza katika halmashauri zote kuhakisha kuwa wakaguzi wa ndani wanakuwa na bajeti yao inayojitegemea tofauti na halmashauri ili kuweza kuboresha hali ya utendaji wao,
Aidha kwa upande wake Raisi wa chama cha wakaguzi wa ndani nchini Tanzania (IIA) Richard Magongo amesema kuwa mkutano huo wa kumi utakwenda sambamba na kushereke miaka kumi tangu kuanzishwa kwa kwa taasisi ya ukaguzi wa ndani.
Amesema kuwa katika mkutano huo wa siku tatu mada mbali mbali zitajadiliwa ambazo kwa kiwango kikubwa kitawqeza kuwasaidia wakaguzi wa ndani katika kuboresha ufanisi wao wa kazi za ukaguzi.
ya mkaguzi
Sambamba na hayo wakaguzi wa ndani wamechangia shilingi milioni tano (5,000,000 )kwaajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera huku Waziri Simbachawene nae akiwaunga mkono kwa kuchangia shilingi laki tano(500,000) taslimu






No comments