Orodha mauaji dada’ke Bilionia Msuya yaongezeka


Marehemu Anneth Msuya.


Dar-es-salaam

 Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya
Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa aliyekuwa
mfanyabiashara maarufu mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,
Erasto Msuya maarufu bilionea Msuya, imeongezeka na kufikia
wawili baada ya mwingine kuunganishwa nayo.

Awali, Agosti 23, mwaka huu mshtakiwa Miriam Mrita (41)
ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa
shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake.

Hata hivyo, juma moja baadaye, mfanyabiashara wa jijini
Arusha, Revocatus Evarist (40), alipandishwa kizimbani katika
Mahakama hiyo na kuuunganishwa na Miriam kwenye kesi
hiyo.

Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa
iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa
Serikali, Diana Lukondo.


No comments