Nyuki Mabingwa Qambalo CUP Karatu

Na.Vero Ignatus.. Karatu.
TIMU ya soka ya Nyuki ya Mang'ola wilayani Karatu mkoa wa Arusha , juzi imetwaa ubingwa wa Soka katika michuano ya Qambalo CUP iliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo,Willy Qambalo baada ya  timu ya mwendokasi magoli 2-1.
Katika michuano hiyo, ambayo ilishirikisha jumla ya timu 55 na wachezaji 1350 kutoka wilaya hiyo ya Karatu, Mabingwa walizawadiwa na Mbunge wa jimbo jimbo  hilo, fedha taslimu sh 400,000 na seri ya jezi.
Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa uwanja wa Karatu, Washindi wa pili walizawadiwa seti ya jezi,mpira na fedha taslimu sh 200,000 wakati mshindi wa tatu  Beach BOYA BOYS
Katika mchezo huo wa  fainali, Nyuki ndio walikuwa wa kwanza kupata gari dk ya 21 goli lilifungungwa na Said  Mustapha  na mwendekasi walisawazisha Dk ya 25 kupitia Nassoro Haji.

Wakicheza kwa kushambulia, nahodha wa timu ya Nyuki  Sadamu Juma alifunga goli la pili dakika ya 33 kwa shuti kali goli lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
Katika michuano hiyo, timu 12 zilipewa zawadiu ya seti ya jezi na mipira baada ya kuingia robo fainali katika michezo iliyochezwa kwenye kata zao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi, Qambalo alipongeza washindi na kuahidi timu bingwa na mshindi wa pili watapata fursa ya kutembelea bungeni Dodoma.
Hata hivyo, alisema michuano hiyo ni utekelezaji wa ahadi zake, katika kuendeleza michezo katika wilaya hiyo ambapo michezo ilikuwa nyuma.
Mwenyekiti wa halmashauri Karatu, Jubilate Mnyenye aliahidi pia kuandaliwa kwa mashindano mengine makubwa ili kuendeleza michezo katika wilaya hiyo.

Katibu na Mbunge wa Karatu, Stivin Siay akikabidhi zawadi ya seti ya jezi kwa nahodha wa timu ya beach boys baada ya kushika nafasi ya tatu.
Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halamashauri ya Karatu Jubilate akikabidhi zawadi kwa washindi hao.

Nahodha wa timu ya Nyuki Sadam Juma akikabidhiwa kikombe na mbunge wa jimbo la Karatu, Willy Gambalo  baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Qambalo CUF.


No comments