Rais Mugabe awaonya mahakimu Zimbabwe


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amewalaumu mahakimu wanaoruhusu
maandamano dhidi ya serikali, ambayo baadae huwa na fujo.

Alisema mahakimu wanadharau amani, na akawaonya kutothubutu kuonesha
dharau wanapofikia uamuzi.

Hapo kesho wafuasi wa upinzani watakwenda mahakamani, kupinga amri
iliyopiga marufuku maandamano kwa majuma mawili.

Kiongozi mmoja wa upinzani, Tendai Biti, amemshutumu Rais Mugabe, kwamba
anajaribu kuwatisha majaji.

Maandamano kadha ya fujo yamefanywa nchini Zimbabwe katika majuma ya
karibuni, huku msukosuko wa kiuchumi ukizidi.



No comments