MKUTANO WA WADAU WA WATALII WAFANYIKA ARUSHA
Na Vero Ignatus Arusha.
Mkutano wa siku moja wa umefanyika Mkoanin Arusha huku wadau w utalii wakiiitaka serikali kuweza kuainisha kodi
zote na kuweka katika mfumo mmoja ili kuweza kuepuka usumbufu
unaojitokeza Mara kwamara pindi wageni wanapokuwa katika matembezi yao.
Wadau hao wamesema kuwa kodi hizo waotozwa katika sehemu mbali hususa ni katika
mageti ambayo wanaingilia watalii mbugani kwani hivi sasa kumekuwepo
na kodi nyingi ambazo zinaleta usumbufu kwa wageni ambapo wanasimamishwa
kila mahali kwa mud a mrefu na kushindwa kufurahia utalii wanaoukuja
kuufanya nchini hapa
Kwa upande wake mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa
utalii (TATO) Wilbroad chambulo wakati akiongea katika kikao cha wadau
wa utalii kilichoandaliwa na mkuu Wa mkoa Wa Arusha cha kujadili
changamoto na tathimini zinazokabili sekta hiyo .
Aliongeza kuwa mgeni anapofika nchini anatakiwa kupokelewa
kama mfalme sio kusumbuliwa kwa kuwekwa mda mrefu katika viwanja vyetu
vya ndege kwani inawakatisha tamaa na kujutia kuja kutembelea vivutio
vilivyopo hapa nchini.
"Unakuta mgeni anakuja akifika kiwanja cha ndege anakaa
zaidi ya lisaa limoja na nusu kwenye foleni akisubiria visa kweli huu ni
usumbufu ,tunatakiwa mgeni akija hapa tumpokee kwa tabasamu ikiwezekana
tumtandikie zulia jekundu ili akienda kwao atangaze nchi yetu na utalii
wetu kwa ujumla "alisema Chambulo.
Pia ameitaka serekali ifutilie na ishughulike na utozwaji
Wa ada za kodi zinazotozwa na mageti ya wilaya ya Monduli pamoja na
geti la wilaya ya Ngorongoro.
"Serekali na Wadau wote tunatakiwa kuweka mikakati
madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama Wa watalii na Mali zao
unaimarishwa zaidi"alisema
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
amesema kuwa mkutano huo ameuita ilikuwaleta pamoja kushiriki na
kujadili namna gani watakuza utalii na kuboresha utalii katika mkoa Wa
Arusha kwa ujumla na iwapo watashirikiana kwa pamoja itasaidia pia
kukuza mapato na kuwa maradufu zaidi.
Amesema nivizuri Wadau Wa utalii wakashirikishwa kwa
mabadiliko yoyote ya ongezeko la kodi ili baadae kusiwepo na malalamiko
ya kuegemea upande mmoja.
Ameongeza kuwa wao kama mkoa wanamkakati Wa kifunga CCTV
katika maeneo mbalimbali ya mkoa ili kuzibiti uhalifu wanaofanyiwa
watalii au wageni wanaotembelea mkoa wetu pamoja na vivutio vilivyopo
Mkoani apo.
![]() |
| Mmiliki wa Leopard Safari Faisal Zuhery akichangia jambo katika mkutano huo wa siku moja wa wadau wa Utalii Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus. |
Katika mkutano huo mambo mambali mbali yaliathimiwa
ikiwemo kuitaka serekali na Wadau Wa utalii kuweka mikakati ya ulinzi na
usalama pamoja na kuangalia jinsi ya kuzuia ujangili.



No comments