MWENYEKITI UVCCM ARUSHA APANDISHWA KIZIMBANI NA VERO IGNATUS ARUSHA
MWENYEKITI
wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha (UVCCM), Lengai ole Sabaya
(29)amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa makosa miwili
ikiwemo kujifanya mtumishi wa umma idara ya usalama wa Taifa (TISS).
Sabaya alifikishwa mahakamani hapo 19 septemba akitokea polisi kisha kuwekwa mahabusu kwa muda na kusomewa mashtaka hayo miwili.
| Mwenyekiti wa Uvccm Arusha Lengai Ole Sabaya picha na Maktaba |
Akimsomea mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama
hiyo, Gwantwa Mwankuga, wakili wa serikali Lilian Mmassy alidai kuwa
kosa la kwanza linalomkabili Sabaya ni la kujifanya mtumishi wa umma
ambapo Mei 18 mwaka huu hoteli ya Sky way iliyopo makao mapya Jijini
Arusha alijifanya kuwa mwajiriwa wa Usalama wa Taifa (TISS).
Kosa la pili katika siku isiyofahamika wala tarehe mwaka
huu alighushi nyaraka za kitambulisho cha usalama wa Taifa chenye picha
yake na kutumia namba Saturday. Code. Eagle 3 idara ya usalama wa Taifa
chenye namba MT. 86117
Hata hivyo Sabaya alikana makosa hayo na ndipo wakili wa
Serikali, Mmassy aliposema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na
dhamana ya mshtakiwa ipo wazi.
Hapo ndipo Wakili wa mshitakiwa, Yoyo Asubuhi alipomuomba
Hakimu Mwankuga kumpa dhamana mteja wake kwakuwa ni haki yake ya msingi.
Naye Hakimu Mwankuga alisema kwakuwa dhamana ipo wazi
anampa masharti Sabaya ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wakuaminika
ikiwemo kusiani hati ya dhamana ya sh, milioni 3 kwa wadhamini wawili kila
mmoja.
Hata hivyo wadhamini hao walikidhi masharti ya dhamana ya
Sabaya na hatimaye kuachiwa kwa sharti la kufika mahakamani kila tarehe
yake kesi na endapo atapata udhuru atoe taarifa mahakamani kupitia kwa
wadhamini hao.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 5 mwaka huu, alipotoka
mahakamani Sabaya alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa hiyo
ni heshima ya kubwa kwake yeye kupelekwa mahakamani ambapo atapata
nafasi ya kuwaumbua wanaopika majungu na fitina.
Amesema wapika majungu hao wamepata nafasi ya kucheza
dakika 45za kutengeneza majungu dhidi yake na anaamini dakika
45zilizosalia zitachezwa ndani ya jengo tukufu la mahakama linalotenda
haki.
Amesema wapo mchwa waliopo ndani ya chama wanaoshirikiana
na upinzani na dunia nzima inawajua na mamlaka husika zimeshindwa
kuwachukulia hatua na kuhoji kwanini mambo haya yabafanyika sasa ikiwa
ni siku chache baada ya aliyekuwa Katibu wake, Ezekiel Mollel kufikishwa
mahakama ya Mwanzo Maromboso na kusomewa shtaka la kufanya vurugu.
Amesisitiza baada ya kutoka mahakamani hapo ataenda ofisi
na kuita kamati ya utekelezaji pamoja na kamati ya uchumi na miradi ili
kumpangia majukumu ya kazi, Said Goha ambaye ni Katibu wa sasa wa Umoja
huo.
No comments