MKUTANO WA WADAU WA UTALII KUFANYIKA ARUSHA KESHO


Na Vero Ignatus Arusha

 Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne  Maghembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku moja wa  wadau wa sekta ya Utalii mkoani Arusha unaotarajiwa kufanyika kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.akisisistiza jambo wakati akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani)ofisini kwake Jijini Arusha, kuhusiana na mkutano wa Wadau wa Utalii utakaofanyika kesho.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake,amesema kuwa mkutano kama huo ulifanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2012 hivyo wameona ni vyema serikali kushirikiana na wadau wa utalii kukaa pamoja kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili  ili kuboresha sekta hiyo,ambayo asilimia 80% ya watalii wanaoingia nchini hufika mkoani hapa .

Amesema kuwa mkoa wa Arusha ni kitovu cha cha utalii na unachangia pato la mkoa kwa asilimia20% na kitaifa kwa asilimia 17%ambapo mwaka 2015 idadi ya watalii iliyoingia nchini ilikuwa 1,137,182 na kuingizia Taifa kiasi cha dola za kimarekani 1.9 milioni,katikaq idadi hiyo asilimia 80%watalii walitembelea mkoa  kwasababu ya vivutio vingi vilivyopo mkoani Arusha.

 
Pichani ni Katibu tawala wa Mkao wa Arusha Richard Kwitega akiwa na wadau wa sekta ya Utalii nyuma yake kama wanavyoonekana pichani wakifuatilia kwa makini wakati Mkuu wa mkoa akizungumza na wanahabari kuhusiana na mkutano wa wadau wa utalii utakaofanyika kesho.picha na Vero Ignatus
Amesema kwamba madhumuni ya mkutano huo ni kujadili hali ya maendeleo ya utalii ya mkoa ,fursa zilizopo,mafanikio ,changamoto na kuweka mikakati yakuboresha huduma mbalimbali za utalii ambapo wadau watapata fursa ya kubadilishana mawazo na kuadhimisha siku ya utalii duiaani amabayo huadhimishwa kila mwaka septemba 27.

“Maadhimisho haya ya utalii  mwaka huu yamebeba kauli mbiu UTALII KWA WOTE,Kwa kuzingatia hilo wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya utalii zikiwemo TANAPA,NCAA,HAT,TTB,TATO,TTGA,TRA,TACTO Watawasilisjha mada ambazo zitalenga kuboresha utalii,pamoja na kuhakikisha elimu na fursa za Utalii zinaifikia jamiii “ alisisitiza Gambo.

Amesema kuwa wadau watakaoshiriki mkutano huo ni wahifadhi,Wakala wa waongozaji watalii,Wakala wa wausafirishaji watalii,watoa huduma za malazi,Bodi ya Utalii,na Viongozi watendaji wa serikali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe.

Mkutano huo wa siku moja umefadhiliwa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA)kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na Ofisi ya Kanda ya Utalii ndiyo waandaaji wa mkutano huo wa wadau mbalimbali wa Utalii Mkoani Arusha

No comments