Mrisho Gambo, afanya mazungumzo na ujumbe kutoka nchini China
Na Vero Ignatus .Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mzungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake hvi karibuni.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mzungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake hvi karibuni.
Amewahakikishia kuwapa ushirikiano,mazingira mazuri
na usalama kwa wawekezaji kutoka China
watakaofika kuwekeza katika Mkoa wa Arusha, na watakapoitaji msaada wowote
kutoka Serikalini basi watapatiwa kwa wakati.
“Kwa Mkoa wa Arusha mtapata ushirikiano
wakutosha kutoka Serikali na mtakapoitaji msaada sehemu yoyote katika utendaji
wenu wa kazi basi msisite kuwasiliana nasi na tutawasaidi”,alisema Gambo.
Aidha mjumbe kutoka ubalozi wa China kwa
Tanzani bwana Gou Huodong,amemwakikishia Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwa ataenda
kuwahamasisha wachina wengine waliopo China kuja kuwekeza zaidi Mkoani Arusha
hasa kwenye sekta ya Utalii ambayo ndio inayokuwa kwa kasi sana na inaongeza
pato la taifa kwa asilimia kubwa.
“Nitaenda kuwahamasisha wenzangu huko China waje kwa
wengi hapa Mkoani Arusha kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbalia hasa ya Utalii
kwasababu sekta hii inakuwa kwa kasi sasa,”alisema Gou.
Pia Muheshimiwa Gambo aliwaelezea mpango
wakufunga Kamera za barabarani(CCTV) kwa Mkoa wa Arusha ilikuimalisha zaidi
ulinzi na Usalama hasa kwa wawekezaji na watalii wanaoingia katika Mkoa huu, na
hivyo kuwaomba waangalie hiyo fursa kwa upande wao iliwaisaidie Serikali katika
kuimalisha ulinzi wake maeneo mbalimbali ya Mkoa.
Ugeni huu kutoka ubalozi wa China hapa nchini
ulikuwa na lengo kubwa lakuweza kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji
yaliyopo katika Mkoa wa Arusha, kwakuwa wageni wengi kutoka China waliofika
katika Mkoa wa Arusha walikutana na mazingira mazuri ya uwekezaji.
![]() |
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipeana mkono na mjumbe kutoka ubalozi
wa China nchini Gou Huodong kama ishara ya ushirikiano baina ya China na
Mkoa wa Arusha.Picha na Vero Ignatus.


No comments