SIKU YA MAMA DUNIANI
Leo ni Siku ya Mama Duniani, siku maalum ya kuwatambua, kuwaenzi na kuwapongeza mama zetu kwa mchango wao mkubwa katika ustawi wa familia, jamii na Taifa letu kwa ujumla. Kwa moyo wa dhati ninawapongeza mama wote kwa kazi kubwa ya malezi mnayoifanya ambayo ni msingi wa Taifa letu kupata raia bora, nguvu kazi mahiri, wataalamu na viongozi.
Tumefanya kazi kubwa, na tunaendelea kuwekeza katika maeneo ya afya ya mama na mtoto, elimu kwa mtoto wa kike, maadili na kuwawezesha wanawake kiuchumi na kisiasa, ili kulinda utu wa mama na kuleta usawa katika fursa zilizopo nchini.
No comments