Nchi 10 zenye nguvu kubwa zaidi za kijeshi Afrika 2025

Nchi 10 zenye nguvu kubwa zaidi za kijeshi Afrika 2025

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jeshi la Umoja wa Afrika
iliofanywa na mtandao wa Marekani wa Global firepower {GFP} ilitathmini nguvu za kijeshi za nchi 145 ulimwenguni, kwa kuzingatia ukubwa wa vifaa, Idadi ya wanajeshi , uwezo wake, fedha, jiografia na rasilimali.

Uwezo huo wa kijeshi unashawishiwa na miungano, uhusiano wa kidiplomasia na hatua zilizopigwa katika teknolojia.

Hapa barani Afrika, Mataifa ya Misri, Algeria, na Nigeria ndio yaliyoorodheshwa katika mstari wa mbele kama yanayoongoza kwa uwezo wa kijeshi yakionesha uwekezaji mkubwa katika bajeti za ulinzi ili kuboresha miundombinu na kupata silaha za hali ya juu.

Mataifa yaliyostawi kiuchumi kama vile Misri na Afrika Kusini yametanguliza matumizi ya ulinzi katika bajeti zake ili kudumisha usalama, huku mataifa mengine yakikabiliwa na changamoto za migogoro ya ndani, vikosi vya kijeshi, na vikosi visivyo na ufadhili wa kutosha kukabiliana na waasi.

Licha ya uwezo wa kikanda, wanajeshi wa Afrika wamesalia nyuma ikilinganishwa na mataifa yaliyoendelea kwa sababu ya tofauti katika ugawaji wa bajeti, teknolojia, mafunzo na ufikiaji wa kimkakati.

Kulingana na Global Firepower, hizi hapa ni nchi 10 za Afrika zenye nguvu kubwa zaidi za kijeshi mwaka 2025.

No comments