Je, nta ya sikio inaweza kufichua maradhi uliyonayo?
Je, nta ya sikio inaweza kufichua maradhi uliyonayo?

Kuanzia magonjwa ya akili hadi saratani, uchafu wa sikio (nta) unaweza kutoa viashiria muhimu juu ya afya ya mtu. Wanasayansi wanachambua nta kwa matumaini ya kupata njia mpya za kugundua magonjwa.
Nta una rangi ya chungwa na unanata. Nta ni mchanganyiko wa nywele, ngozi iliyokufa na uchafu mwingine. Mara baada ya kuundwa kwenye mfereji wa sikio, husafirishwa kutoka ndani ya sikio hadi nje.
Faida za Nta
Miongoni mwa sababu za kuzalishwa nta ni kuuweka mfereji wa sikio safi na kuulainisha. Pia hutumika kama mtego, kuzuia bakteria, kuvu na wadudu wengine kutoingia katika sikio.
Faida ya hayo, kutokana na tafiti kadhaa za kisayansi - nta sasa unaweza kutumika kugundua aina fulani ya habari za maana na muhimu kuhusu afya ya binadamu.
Chanzo BBC
No comments