Ifahamu mimea mitano inayolindwa zaidi duniani
Ifahamu mimea mitano inayolindwa zaidi duniani

Chanzo cha picha,Getty Images
Kila mwaka, zaidi ya makontena milioni 240 husafirishwa kati ya nchi na nchi, yakiwa na bidhaa za mimea, na kuongeza hatari ya usalama wa mimea na viumbe hai. Kwa mantiki hiyo ulinzi wa mimea umekuwa ni jambo linalopewa kipaumbele na dunia, kwa sababu ya umuhimu wake kwa uhai wa binadamu.
Kila tarehe Mei 12, dunia huadhimisha Siku ya Afya ya Mimea iliyoanzishwa ili kuhamasisha umuhimu wa kulinda afya ya mimea kwa ajili ya uzalishaji endelevu wa chakula, ulinzi wa mazingira na uchumi wa dunia.
Tunakuletea mimea mitano kati ya mimea kadhaa inayolindwa kwa kiwango cha juu duniani.
Mimea hii si tu adimu, bali pia ina umuhimu mkubwa wa ikolojia, kihistoria na hata kitamaduni.
Mataifa na mashirika kadhaa dunia hutumia mabilioni ya fedha kuhakikisha afya na uhai wa mimea hii.
Na watetezi wa mimea wanatoa wito wa kulindwa kwa mimea hii kama yanavyolindwa madini ya almasi
No comments