ZAHANATI YA KAMSISI HALMASHAURI YA MLELE INATAZAMIWA KUHUDUMIA WANANCHI 12,215 PAMOJA NA VIJIJI JIRANI


Na. Mwandishi wetuKatavi

Wananchi wa kijiji cha Kamsisi kilichopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wameishukuru Serikali kwa ajili ya kushirikiana nao kujenga Zahanati itakayohudumia wananchi 12,215 wa kamsisi na vijiji jirani vya Imalauduki na Songambele ambavyo hazina Zahanati.

Kauli hiyo waliitoa kwa Nyakati tofauti wakati walipokuwa wakizungumza na Mwandishi wa habari hizo kuhusiana na maendeleo ya kata yao kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mlele.

Matha Zalote ni mmoja wa wanakijiji alisema kuwa kuwepo kwa Zahanati hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na usumbufu wa kusafiri umbali wa kilometa 12 kutoka kijijini hapo hadi wilayani kufuata huduma za Afya.

Kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo itawasaidia jamii kwa ukaribu na  kuondokana na akina mama kwani wengi wao ujifungulia njiani huku wakitembea umbali mrefu.

Kuwa kutokana na kero hiyo  waliamua kuanza kushirikiana na Halmashauri juu ya kuchangia maendeleo ikiwa ni moja ya mafunzo waliyopewa hivyo  waliona ni vyema kuanzisha Zahanati hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwao 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlele ,mwalimu Alexius Kagunze alisema kuwa Halmashauri imelenga kushirikiana na jamii katika kuchangia maendeleo ya jamii kwa manufaa ya Taifa zima ambapo wananchi wanapaswa kujitolea na Halmashauri kuwaunga mkono .

Kuwa Mradi huo wa jengo la  Zahanati unajumuisha Nyumba ya mganga na matunda manne ya vyoo ambapo hadi kukamilika zaidi ya kiasi cha shilingi Milioni 86 zinahitajika huku zaidi ya shilingi nilion 64 ni nguvu za wananchi ,na kiasi cha zaidi ya milioni 20 ni usaidizi wa Serikali Kuu kupitia mfiko wa kychochea maendeleo ya Jimbo.

Aliongeza kuwa zaidi ya Shilingi milioni 1 kimetolewa na Halmashauri huku akidai kuwa hadi kufikia hatua hiyo tayari kiasi cha Shilingi zaidi ya milioni 54 zimetumika na kwamba kukamilika kwa Mradi huo kutawapatia fursa ya kupata huduma bora za Afya kutokomeza malaria na kujitambua kupima katika harakati za kupunguza maambukizi mapya ya ukimwi katika kijiji cha Kamsisi.



Mwisho.

No comments