RAIS MHE. DKT MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI IRINGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.

Wafanyakazi mbalimbali wakipita kwa maandamano katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.

Sehemu ya Wafanyakazi waliohudhuria katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi mara baada ya kuhutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na wasanii wa kizazi kipya kutoka mkoani Iringa waliotumbuiza katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.

Sehemu ya Walimu waliohudhuria katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa wakipiga makofi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiwa na Chifu wa Wahehe, Mtwa Adam Mkwawa II ambaye alihudhuria katika katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiondoka katika uwanja wa CCM wa Samora mkoani Iringa mara baada ya kuhutubia katika shere za Mei Mosi.
PICHA NA IKULU
''Kipindi changu cha Urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara wafanyakazi. Na mimi nataka niwaeleze kupandisha kwangu kutakuwa si kwa elfu kumi, kutakuwa kupandisha kwelikweli'', amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameweka wazi kuwa alitamani sana mwaka huu kupandisha mishahara lakini baada ya kuona changamoto zilizopo ikiwemo kulipa madeni ya nyuma akaona azimalize kwanza kabla ya kupandisha.
"Natamani mwaka huu kupandisha mishahara kwa wafanyakazi lakini kutokana na changamoto zilizopo za kuajiri wafanyakazi 52,000 nitawalipa nini? nikisema natamka kuongeza mishahara, nitazipata wapi?”amesema Magufuli.
Pamoja na hayo Rais Magufuli ameviomba vyama vya wafanyakazi na masharikisho yao, kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwasababu inaongozwa na walimu akiwemo yeye mwenyewe na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao wote wamewahi kuwa walimu.
Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya, kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo ambazo zimefanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.








No comments