Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) yaadhimisha siku ya uguru wa habari


Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) Mei 3,2018 imeungana na waandishi kote duniani kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 3 Mei.

Maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na wadau wa habari mkoani Shinyanga yamefanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack aliyekuwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.

Maadhimisho hayo ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga yaliyokuwa yanarushwa moja moja 'Live' na Radio Faraja Fm Stereo pia yamehudhuriwa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari nchini - UTPC, Salma Abdul.

Maadhimisho ya siku hii kitaifa yamefanyika jijini Dodoma lakini kwa mujibu wa mwongozo wa wasimamizi wetu UTPC mwaka 2018 kila Klabu imeelekezwa kuadhimisha siku hii kwa ngazi ya mkoa na Kauli mbiu ya klabu zote ni ‘Uhuru wa habari ni chachu ya uwajibikaji wa maendeleo ya mkoa’.

No comments