RC DKT. KEBWE AAGIZA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI GAIRO WAKAMATWE
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea maelezo ya wizi
wa pampu ya maji kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe
katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe ili kuweza kuwalejeshea
wanachi maji. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema nashangaa kuona
pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu
miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo
ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako
wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja.
Kisima kilichoibiwa pampu.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakitoa pole kwa wafiwa wilayani katika kijiji
cha Tabuhoteli -Gairo wakati wa ziara yake ya siku tatu anayoifanya ili
kuchochea maendeleo shughuli za maendeleo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Tabuhoteli katika kata ya Chigela - Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa salamu zake kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakiongoza wananchi kuelekea katika mradi wa
maji wa Ihenje.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakipokelewa kwa ngoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo
Mhe. Siriel Mchembe wakimsikiliza Mhandisi wa wilaya ya Gairo, Heke
Bulugu wakati akitoa maelezo ya 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akitoa neno la shukrani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wananchi.
GAIRO.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.
Kebwe Stephen Kebwe ameliagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo
kuwatafuta na kuwakamata watu walioharibu miundo mbinu ya maji ikiwemo
kuiba pampu ya maji ya Kijiji cha Italagwe katika Wilaya ya Gairo na
kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.
Dkt.
Kebwe ametoa agizo mapema leo Mei 24 mwaka huu akiwa katika Kijiji cha
Italagwe Kata ya Italagwe, wilayani humo wakati wa ziara yake ya siku
tatu ya kutembelea na kuhimiza miradi ya maendeleo katika Wilaya ya
Gairo Mkoani Morogoro.
Amesema
kuwa changamoto kubwa inayowakumba wananchi wa Wilaya ya Gairo ni
pamoja na tatizo la maji, hapati majibu sahihi kuona pamoja na
changamoto hiyo bado kuna watu wanaodiliki kufanya hujuma ya kuiba
miundo mbinu ya maji na kuwasababishia wengine kukosa maji. "Nashangaa
sana kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado
wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba
Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD
ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane
mara moja," amesema.
“OCD
Mkong’oto utembee kwenye kijiji hiki. Mkong’oto utembee pampu ipatikane.
Kuna wengine watachukulia kisiasa siasa suala hili, hiyo ndiyo kazi ya
Mbunge kuangalia kwamba tunachangamoto gani asaidiane na wananchi”
alisema Dkt. Kebwe “wezi wapo hapa hapa kijijini. DC banana na Afisa
Tarafa, Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji, fanyeni Mkutano wa hadhara
pampu ipatikane” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa, mradi huo wa maji ulianza mwaka 2014 hadi
2015 ambapo uligharimiwa na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahmed Shabiby
na ulihudumia vitongoji viwili vya Dukani na Chang’ombe vyenye watu
wasiopungua 2,500 na Oktoba mwaka 2017 mradi uposimama kutoa huduma kwa
sababu ya pampu hiyo kuibiwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchemba amewahakikishia wananchi wa Gairo
kuwa changamoto ya Maji wilayani humo inakaribia kuisha kwa kuwa
takwimu pamoja na utekelezaji unaonesha upatikanaji wa maji unaongezeka.
Upatikanaji wa maji mjini umeongezeka kutoka asilimia 35 hadi asilimia
40.7 na vijijini umefikia asilimia 51.4 kati ya asilimia 85
zinazohitajika hivyo mradi wa maji wa MORUWASA utakapokamilika
changamoto ya maji Gairo itakuwa ni ndoto.
"Nawaomba
wananchi wangu wa Gairo waendelee kuwa wapole maana kila kukicha
tunajaribu kutatua changamoto zinazotukuta likiwemo hili la maji ambalo
halitachukua muda mrefu tutakuwa tumelimaliza kabisa," amesema.
Mhe.
Mchembe ameongeza kuwa wanawake wanaweza hivyo waendeee kuwaamini
hawatawaangusha wananchi, "Wilaya yetu inaongozwa asilimia 70 inaongozwa
na akinamama hivyo tunajua changamoto zinazokuba ikiwemo zile za
majumbani.. vumilieni yatakwisha'.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe bado anaendelea na ziara yake
Wilayani Gairo kwa lengo la kutembelea na kuhimiza utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo na kupokea kero za wananchi.
No comments