Afisa Itifaki mkoa wa Arusha apandishwa kizimbani

Na. Vero Ignatus Arusha. 

AFISA Itifaki katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Swalehe Mwidadi (32) na mtumishi wa idara ya masijala Amina Mshana 29 wote  kwa pamoja wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Arusha kwa kosa la unyang’anyi wa matendo ya ukatikli na udhalilishaji dhidi ya mwandishi huyo.

Wathumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kumteka mwandishi wa habari Lucas Myovela na kumpora mali zake mbalimbali zikiwemo simu za kiganjani na kadi za benki

Akiwasomea mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali   Sabina Silayo aliileza mahakama mbele ya hakimu Paricia Kisinda kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Mei 13 mwaka huu

Wathumiwa hao wanadiwa kupora kwa kutumia silaha za jadi kuchukua simu yake ya kiganjani aina ya Tecno C 7 yenye thamani ya shilingi 300,000.

Mali nyingine za Myovela walizopora watuhumiwa hao ni pamoja na simu nyingine ya kiganjani aina ya Sumsung yenye thamani ya shilingi 50,000, fedha shilingi 75,000 .shilingi 9,500 kutoka kwenye simu yake kiganjani

Kosa la pili linalowakabili watuhumiwa hao  ni matendo ya ukatili na udhalilishaji ambapo walimvua nguo Myovela  na kuanza kumchukua picha za video akiwa uchi.

Baada ya maelezo hayo watuhumiwa walirejeshwa rumande na kesi kuahirishwa hadi juni sita mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika
Afisa Itifaki katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha (wa kwanza kulia) Swalehe Mwindadi akiwa mahakamani leo, kutokana na kesi inayomkabili ya kumteka mwandishi wa habari mkoani hapo. Mei 13/2018katika eneo la Sakina. 
Mtuhumiwa anayedaiwa kuhusika kumteka mwandishi wa habari Jijini Arusha bi Amina Mshana@loveness anayefanya kazi ofisi ya masijala ofisi ya mkuu wa mkoa akiwa mahakamani leo 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa nje ya Mahakama wakisubiria kusikilizwa kwa kesi hiyo. 



No comments