TCRA WATOA LESENI KWA WATOA HUDUMA ZA HABARI MTANDAONI
*Mkurugenzi TCRA asema 45 ndio wamekidhi vigezo kati ya waombaji 262
*Asema mchakato bado unaendelea, atoa sababu kuweke gharama za usajili
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAMLAKA
ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania(TCRA)imesema leo ni siku muhimu
katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na kushuhudiwa wadau wa
habari wakiwa wamekamilisha hatua za usajili ili watambulike na kutumia
fursa hiyo ya utoaji na upashaji habari kupitia mtandao wa intanenti.
Kutokana
na kukamilisha mchakato huo TCRA imetoa leseni kwa watoa huduma wa
maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti 45 kati ya watoa huduma 262
walioomba na kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa.Miongoni mwa
waliopewa leseni baada ya kukamilisha taratibu hizo ni pamoja na Michuzi
Media Group(MMG)
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi
James Kilaba wakati akikabidhi cheti cha usajili kwa wamiliki 45 wa
Blogs, Redio na televisheni za mtandaoni na kusema kuwa zipo faida
nyingi za habari na utangazaji kwa njia ya mtandao ambazo zinafahamika
kwa wengi.
"Kama
tunavyofahamu kwa miongo mingi sasa sekta ya habari na utangazaji
imekuwa ikipata habari kwa njia ya redio na televisheni kupitia majukwaa
mbalimbali kama mitambo iliyojengwa ardhini,Satellite na Cable.
"Baadae
kwenye miaka 2000 teknolojia ya intaenti iliingia ingawa matumizi yake
yalikuwa kwa ajili ya mawasiliano ya kawaida kama vile barua pepe bila
kujumuisha matumizi ya vyombo vya habari (online media
service),"amesema.
Ameongeza
ujenzi wa mkongo wa Taifa nchini unaotumia "optic fiber" na matumizi ya
teknolojia ya 4G vimechangia ongezeko la kasi ya usafirishaji wa
taarifa ya vyombo vya habari (broadband) na kuwezesha matumizi ya habari
mitandaoni.
Ameeleza
kuanzia mwaka 2013 Watanzania wameshuhudia kuongezeka kwa kasi kwa
vyombo vya habari mtandaoni hata kuleta mvuto wa pekee kwa wananchi
wengi na kupelekea fursa kwa kila mmoja na kuleta mapinduzi chanya
kwenye sekta ya habari na utangazaji hasa kwa wanaoitumia vema.
"Zipo
faida nyingi za habari na utangazaji kwa njia ya mtandao ambazo
zinafahamika.Mojawapo kubwa ni kutoa fursa ya ajira kwa wengi hasa
vijana. ambapo baadhi yenu hii imekuwa chanzo cha mapato kwa ajili ya
kurahisisha maisha.Faida nyingine ni upatikanaji wa habari kwa haraka
hasa za matukio mbalimbali yanayotokea miongoni mwa jamii,"amesema.
Amefafanua
matumizi bora au mabaya ya mawasiliano yanaweza kufanyika kwenye
majukwaa hayo ikiwa hayatakuwa na utaratibu mzuri uliowekwa kuhusu
maudhui. Hivyo ni kwa ajili hiyo Serikali imeendelea kuwa na sheria na
kanuniz zinazosimamia majukwaa hayo ambayo yamekuwa yakitumika na
yanayoendelea kutumika ili kuhakikisha kuna matumizi bora na salama
kwenye tasnia ya habari na utangazaji kwa watoa huduma na watumiaji.
"Hali
kadhalika kwasababu zile zile mawasiliano kwa njia ya mtandao kwa
vyombo vya habari nayo yanatakiwa kuwa yanatumika vema ili kuwa na
matumizi bora na salama. "Ni matumaini yangu wote tunakiri na kuona haja
ya majukwaa haya yanakuwa na utaratibu mzuri kupitia sheria na kanuni
.Hivyo usimamizi wa matumizi bora ya majukwaa haya ni muhimu bila
kubagua kwa vile yote yanabeba maudhui kwa ajili ya
mawasiliano,"amesema.
Amefafanua
kwa kuzingatia umuhimu huo Serikali ikaandaa kanuni za maudhui
mtandaoni za mwaka 2018 zilizoanza kutumika Machi mwaka 2018 na kuongeza
kanuni nne inaipa uwezo TCRA kufanya mambo muhimu matatu. Ameyataja ni
kutuza rajis ya wanablogu , majukwaa ya habari mtandaoni , redio na
televisheni mtandaoni.Pia kuchukua hatua dhidi ya wakiukaji wa kanuni
hizo ikiwemo kuagizwa kuondolewa kwa maudhui yaliyokatazwa na kuelimisha
umma kuhusu salama ya maudhui mtandaoni.
Mhandisi
Kilaba amesema katika kutekeleza matakwa ya kanuni hizo za maudhui
mtandaoni za 2018 wamekamilisha taratibu rahisi za kuwasilisha maombi ya
usajili tangu Aprili 21 mwaka huu na hivyo kuwezesha mwanzo wa kuwa na
rajis endelevu ya wanablogu, majukwaa ya habari mtandaoni ,redio na
televisheni mtandaoni. Amesema kuongezeka kwa orodha ya wanaotambulika
itakuwa chachu kubwa katika ushirikiano wa kuhabarisha na kuelimisha
umma. Pia amesema usimamizi wowote wa sekta una gharama zake ili
kuhakikisha kuwa huduma inayotolewa inakidhi matarajio ya watanzania
wengi.
Amesema
gharama zilizopo zinalenga kuzuia uanzishwaji holela wa vyombo vya
habari mtandaoni usiokidhi viwango vinavyotakiwa, kuleta ushindani sawa
wa vyombo vya habari na kutambua watu wenye nia safi ya kutoa huduma
hiyo ya maudhui mtandaoni kwa jamii. "Naomba nitumie fursa hii
kuwakumbusha kwamba si nchi yetu ya Tanzania pekee iliyokumbwa na
changamoto za matumizi na habari salama mitandaoni kisha kuchukua
hatua.Huko duniani hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa kulingana na
tamaduni, mila ,desturi na mahitaji ya nchi husika.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa
njia ya mtandao , iliyofanyika leo katika ukumbu wa TCRA jijini Dar es
Salaam.
Katibu
wa Chama cha Wamiliki wa Blogers , Krants Mwantepele akizungumza
kuhusiana na mwitikio ulionyeshwa kwa wamiliki kujisajili TCRA
iliyofanyika , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa
Mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group (MMG), Ainde Ndanshau katika
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa
Mkurugenzi wa Blogu ya Wananchi , William Malecela ‘LE MUTUZ ‘ Vkatika
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa
Mwakilishi wa Mtandao wa Bongo 5, Yassin Ng’itu katika hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa
Mmiliki wa Habari Mseto , Francis Dande katika hafla iliyofanyika katika
ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa
Mmiliki wa Radio Seven ya Mtandaoni, Atu Mandoza katika hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi na wamiliki wa watoa huduma kwa njia ya mtandao
No comments