TANZIA; MJUMBE WA BODI YA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), BW. ATHUMANI HAMISI AFARIKI DUNIA


MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Athumani Hamisi, amefariki dunia mapema leo Januari 4, 2017.

Taarifa zilizopatikana leo jijini Dar es Salaam, Bw. Hamisi ambaye pia aliwahi kuwa mpiga picha mkuu wa magazeti ya Serikali, (TSN), atazikwa kesho Ijumaa Januari 5, 2018 kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na msiba uko nyumbani kwake Sinza Madukani.

Kwa muda mrefu, Bw. Hamisi alipatwa na ulemavu baada ya kupata ajali mbaya wilayani Kibiti alikokwenda kikazi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi AMIN.


No comments