Mkuu wa wilaya Mbeya Ntinika awataka Waandishi wa habari kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria taratibu na Maadili ya Kihabari

Makamu mwenyekiti wa CHama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (MBPC )Hosea Cheyo,akitoa ufafanuzi katika mkutano uliofanyika leo.
Mkuu wa wilaya ya MbeyaWilliam Ntinika akisisitiza jambo katika mkutano wa klabu ya waandishi wa habari Mkoani Mbeya (MBPC) uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Gadern mkoani hapo.
Mkutano mkuu wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Mbeya ukiwa unaendelea 

Na.Mwandishi wetu Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,William Ntinika amewapongeza waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya(MBPC)kwa kufanya mkutano Mkuu hali itakayoendelea kuwaweka pamoja,kujadili utendaji wao wa kuhabarisha umma kwa kuzingatia weledi na maadili ikiwemo  namna ya kujipanga vyema kwa mwaka 2018.

Akifungua Mkutano huo leo,uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden,jijini Mbeya ,Mkuu wa Wilaya,Ntinika amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli na wasaidizi wake ipo bega kwa bega na wanahabari na inatambua mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Aidha Mheshimiwa Ntinika amewaondoa hofu waandishi wa habari kuwa wapo salama muda wote katika majukumu yao ya kila siku huku wakiwataka kufanyakazi kwa mujibu wa sheria na taratibu na maadili ya kihabari.

"Serikali ya Rais Magufuli,na sisi wasaidizi wake kuanzia Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya tunawaunga mkono katika maendeleo ya Taifa,tunatambua mchango wenu mkubwa na ndiyo maana tumekuwa tukiwashirikisha katika matukio mbalimbali kwa kuwaalika ili  jamii iweze kujuwa na kupata taarifa ya nini kinachofanyika kwa maslahi yao," alisema.

Ntinika aliendelea kufafanua kuwa,wasemaji wakuu wa Serikali kwa ngazi ya Mkoa ni Mkuu wa Mkoa na ngazi ya Wilaya ni Mkuu wa Wilaya,"tuzingatie hilo na endapo mtapokea vitisho na hofu ya usalama wenu tupigieni simu na Kamati ya ulinzi na usalama ipo kwa ajili ya kulinda usalama wenu na raia wote alimradi sheria isivunjwe."

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti,Hosea Cheyo ametoa taarifa ya muendelezo wa muda wa  kuwepo  madarakani kwa muda wa miaka mitano.
"Mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba,Katiba ni Sheria Mama ya UTPC,Katiba inatoa mwelekeo wa namna gani

No comments