Mpango Maalum wahutajika kutoa Elimu kwa waandishi kuubya Uhifadhi na Italii

Mwenyekiti wa Waongoza Utalii nchini TTGA Khalifa Msangi akitoa mada juu ya majukumu na Changamoto kwa waongoza watalii nchini,katika Kongamano la wanahabari Kanda ya Kaskazini.

Taasisi ya wanahabari Media imefanya Kongamano na waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini,likiwana lengo la kuwajengea uwezo wankuandika vyema habari za Utalii na Uhifadhi.

Akifungua kongamano hilo Katibu Tawala mkoa Arusha Richard Kwitega alisema serikali inathamini mchango wa wanahabari katika kukuza na kutangaza utalii.

Amesema kuwa Serikali kupitia wizara ya Maliasili inaendelea na mikakati kuitangaza vyema Tanzania, kutangaza vivutio na kuendeleza uhifadhi

Afisa Utalii mkoa wa Arusha Flora amesema wadau wa utalii nchini wanatakiwa uweka mpango maalum ambao utatoa elimu kwa waandishi kuhusiana na uhifadhi na utalii

 Kwitega amesema kwa sasa kero nyingi zinafanyiwa kazi ikiwepo kuondoa kero kwa watalii na wadau wa utalii,kuimarisha usalama wa watalii nchini itakayotaliwa

 Tozo ambazo zilikuwa kero za watalii Arusha zimeondolewa na hali ya usalama ni nzuri

Kwa upande wake  Katibu wa jukwaa la Wahariri Nelvin Meena alisema wanahabari ni nguzo muhimu katika kukuza sekta ya utalii


No comments