Asilimia 95 ya wageni wanaoingia Nchini kutembelea Hifadhi ni kutoka nje ya Nchi
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Naibu waziri wa Habari sanaa,utamaduni na michezo Juliana Shoza amesema kuwa asilimia 95 ya wageni wanaotembelea katika hifadhi za wanyama na vivutio vilivyopo nchini ni wageni kutoka nje ya nchi.
Ameyasema haya katika uzinduzi wa Kongamano la Tanzania Tukuza Utalii genesis 1 Jijini Arusha ambapo amesema kuwa watanzania waonyeshe Uzalendo kwa kupenda vya kwao na kutukuza vya kwao.
Amewataka vijana kuwa wazalendo kwa taifa lao kwa kufanya kazi kwa bidii kwa wale waliopo katika shughuli mbalimbali,na kwa wanafunzi wasome kwanbidii kwani Elimu ndiyo itakayowakomboa.
Amewataka wasanii kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuvaa nguo za kujistiriri kwani atakayekiuka serikali haitamfumbia macho
Katibu mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Godfrey Mngereza..
Katibu mkuu mtendaji kutoka Baraza la sanaa nchini (Basata ) Godfrey Mngereza amesema kuwa sanaa ni eneo ambalo limekumbwa mmomonyoko wa maamdili, hivyo amewataka wasanii wote kutunza na kulinda maadili ya Kitanzania kwani sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.
Amesisitiza kuwa sanaa ni nyenzo hivyo huwezi kutenganisha utalii na sanaa,kwani vinatumika kutangaza utalii wa Mtanzania na vivutio vilivyopo na utalii
Amesema watoto lazima wafundishwe misingi ya sanaa,kwamba sanaa ipo kwa upana wake na sanaa ina heshima,pia msanii ni kioo cha jamii na asitumike kuichafua.
Kwa upande wake Rais wa Mtandao wa wasanii wa nyimbo za Injili na Maadili Tanzania (Tagoane )Dkt.Godwin Maimu amesema kuwa kutokana na tathimini aliyoifanya katika shule mbalimbali amebaini asilimia 93.7 ya wanafunzi wameona wanyama kupitia luninga na kwenye machapisho mbalimbali.
Amesema kuwa ipo hatari kama taifa kuna vitu ambavyo Mungu amewapatia wasipojengewa msingi imara wa kuvifahamu ,wanauwezekano mkubwa wakutokuijua Tanzania yao na kuifaidi pamoja na vivutio mbalimbali vilivyopo.
No comments