Dr.MITIMINGI: SIJTOKA TAG KWA UGOMVI, AJA NA WCC KWA KISHINDO

Mchungaji na Mwalimu Dkt.Peter Mitimingi akiwa anahubiri katika Ibada ya Uzinduzi wa Kanisa la Ghala la Chakula cha Uzima (WCC) Katika ukumbi wa hoteli ya Kebbys Jijini Dar es salaam.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus Dar es salaam

Baada ya kutumika katika kanisa la Tanzania Asseblies of God  (TAG ) zaidi ya miaka ishirini Mchungaji na mwalimu Dr Peter Mitimingi azindua kanisa lake rasmi leo Kebbys Hotel Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi wa kanisa hilo uliohudhuriwa na zaidi ya watu elfu tatu  Dr Mitimingi amesema kuwa yapo malengo matatu ambayo yamepelekea yeye kuanzisha WCC ikiwa ni pamoja watu kukua kiroho ,wawe na Ufahamu,waijue kweli ambao utamsafirisha kupata majibu ya changamoto mbalimbali pamoja na Uhuru

Amesema kuwa wengi waneokoka na wapo makanisani miaka mingi lakini hawajakua kiroho,amesema kuwa mtu akilifahamu tatizo ni jibu sahihi kuliko kutokujua tatizo.

"Kwakutolifahamu tatizo unaweza ukatibu ugonjwa ambao siyo kabisa ila ukilifahamu tatizo utajua uanzie wapi kulitatua,kwani ratizonlinaanzia kwenye kulijua tatizo lenyewe " alisema Mitimingi

Ambapo ameeleza kuwa katika malengo hayo endapo angeendelea kuwa katika kanisa la TAG malengo hayo yasingekamilika kutokana na taratibu za Kanisa hilo.

"Sijatoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG )kwa ugomvi kama watu wanavyozusha bali nilikwenda kwa viongozi wa juu wa Kanisa wakanisa nilianza na nyumbani Mwenge TAG
ambapo nilikuwa mchungaji msaidizi,nikaenda kwa mchungaji wa wilaya ,nikaenda kwa Makamu wa Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dkt.Magnus Mhiche ,wote hawa walinikubali ,wakaniombea na kuniwekea mikono tayari kwa kutumika." Alisema Mitimingi. 
 
Mwalimu na Mchingaji Dkt.Peter Mitimingi akiwa anamuombea mtoto mara baada ya kumalizika uzinuizi wa Kanisa la WCC Jjini Dar es salaam.Picha na Vero Ignatus Blog.

Mchungaji na Mwalimu Dkt.Peter Mitimingi akiwa na mkewe Subira Mitimingi   waanzilishi wa Kanisa la Ghala la chakula cha Uzima (WCC) lililozinduliwa Jijini Dar es salaam.Picha na Vero Ignatus Blog.

Timu ya Wahudumu wa kanisa la WCC pamoja na kundi la waimbaji wa Sifa na Kuabudu wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji,Mwalimu Dr kt.Peter Mitimingi.

Baadhi ya watu mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Kanisa laa WCC Jijinj Dar es salaam.Picha na Vero Ignatus.


Watu mbalimbali waoiohidhuria katika uzinduzi wa Kanisa la WCC wakiendelea kuatilia kinachendelea kwa makini .Picja na Vero Ignatis Blog.
 
Ukumbi ambao uzinduzi wa Kanisa la WCC ulifanyika na ndipo ibada zitakuwa zikifanyika.Picha na Vero Ignatus Blog.





No comments