MANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO KESHO JUMAMOSI KATA YA KIMANDOLU YAMEKAMLIKIA

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Arusha Mjini ambaye ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura katika marudio ya uchaguzi mdogo
unaorudiwa kesho jumamosi kwenye kata ya Kimandolu Jijini Hapa.
Akizungumza na Kusaga News Blog Kihamia amesema kuwa vifaa vyote viko tayari na vimefika kwenye vituo vyote 34 vilivyopo katika kata na vitafunguliwa kesho saa moja kamili mpaka saa kumi kamili jioni.
“Kesho ni uchaguzi tumeshajipanga vizuri kwa maana ya mandalizi vifaa pamoja watendaji wa uchaguzi tunasubiri tu muda ufike uchauzi huu unafanyika kesho siku ya jumamosi tarehe 13 januari 2018 na siyo jumapili kama wananchi wengi walivyozoea siku za nyuma kwahiyo tunataka kuona uchauzi huu unaenda vizuri na vituo vinafunguliwa keshoo saa mbili kamili asubuhi”Amesema Kihamia
Kihamia amesema kuwa wananchi watakapopiga kura waondoke majumbani kwao kwa kuwa hali ya ulinzi imeimarishwa hivyo wasiwe na hofu yeyote.
Hata hivyo amesema kuwa kwa watu waliopoteza vitambulisho vyao vya kupiga kura wanaweza kutumia leseni ya Udereva,kitambulisha cha taifa NIDA,au paspot ya kusafiria na jina liwe kwenye orodha ya majina ya wapiga kura.
“Wapiga kura walioko kwenye daftari wanakaribia elfu 16 kitu ambacho ni muhimu kila kitu kiko sawa mawakala wote wameapishwa wa vyama vyote na kuna vyma vitano ambavyo ni CCM,NRA,CUF,SAU,DEMOKRASIA MAKINI ,NRA na mwisho wa kupiga kura ni saa kumi kamili lakini atayekutwa yuko kwenye foleni katika muda huo basi atapiga kura”Amesema
Majimbo 3 yanatarajia kurudia uchaguzi ambayo ni Londigo,Singida ,Singida Kaskanini,na Songea Mjini kata 6 ambazo ni Kimandolu (Halmashauri ya Jiji la Arusha), Kihesa (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa), Bukumbi (Halmashauri ya Wilaya ya Uyui), Kurui (Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe), Keza (Halmashauri ya Wilaya ya Ngara) na Kwagunda (Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe
No comments