Wasafirisha Taka Dodoma walalamika Ubovu wa Barabara

Waandishi wa habari za Mazingira wakiwa katika eneo la mapokezi katika eneo la Dampo la Chidaya Dodoma.Picha na Vero Ignatus Blog.
Waandishi wakipokea maelekeza kutoka kwa muwezeshaji wa mafunzo Deodatus Mfugale.Picha na Vero Ignatus Blog.
Waandishi wa habari za Mazingira wakielekea mahali ambapo Dampo lilipo na kuona namna ambavyo limetengenezwa kwa kisasa tofauti na Madampo ya kawaida.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wakiwa katika eneo la juu ambapo hatua chache ndipo takataka zikiletwa zinamwagwa .Picha na Vero Ignatus Blog.
Waandishi wa habari wakiwa katika eneo la Dampo la kisasa la Chidaya mkoani Dodoama .Picha na Vero Ignatus Blog.
 Baadhi ya Gari la Almashauri likiwa linapeleka taka kwenye Dampo hilo .Picha na Vero Ignatus Blog
Muonekano wa Dampo Jipya la Chidaya lililopo mkoani Dodoma .Picha na Vero Ignatus Blog.
Mzani wa kupimia magari yanayoleta taka katika Dampo la Chidaya.Picha na Vero Ignatus Blog.
Waandishi wakiwa katika eneo la kukagulia taka kabla ya kupelekwa kumwagwa kwenye Dampo .Picha na Vero Ignatus Blog.

Na,Vero Ignatus Dodoma

Wasafirishaji wa takakataka mkoani Dodoma wamelalamikia ubovu wa barabara iendayo kwenye Dampo la Chidaya mkoani hapo.

Akizungumza na jopo la waandishi wa habari za mazingira waliotembelea dampo hilo mmoja wa wasafirishaji hao Godgrey Chorobi  amesema kuwa bovu wa barabara hiyo unasababisha magari ya kuzolea taka kuharibika mara kwa mara hivyo kuwaingizia gharama za ziada ambazo zimekuwa hasara kwao 

Amesema kuwa mwisho wa siku gharama hizo za ziada zitalipwa na wananchi hali itakayosababisha wananchi wengi kushindwa kumudu gharama za taka

"Barabara hadi dampo ni mbovu sana,magari yanaharibika sana na tunalazimika kuingia gharama za ziada hivyo tunaomba mamlaka zinazohusika ziliangalie suala hili na kuzitengeneza barabara hizi"alisisitiza

Hata hivyo katika hali ya kushangaza ,pamoja na barabara hiyo kuwa mbovu yenye vumbi baadhi ya wananchi hao wameitaka serikali isikarabati barabara hiyo badala yake dampo hilo lihamishwe hadi kufikia umbali wa kilometa 60 kutoka mjini Dodoma ili kuendana na ukuaji wa kasi wa mji huo mkuu wa Tanzania


Amesema licha ya umbali mrefu kilometa 12 kutoka katikati ya mji wa Dodoma hadi kulifikia Dampo hilo ni changamoto hiyo ya barabara mbovu huku akiomba uongozi wa manispaa ya Dodoma kufikiria kuweka lami barabara hiyo badala ya kuwa na kero kwa wadau wa kuzoa taka.

Ubovu wa barabara hiyo  ni kikwazo kwa baadhi ya watu kupeleka taka sehemu inayostahili  hivyo kufanya ujanja wa kuzitupa taka hizo kwenye maeneo ambayo siyo rasmi.

Mmoja wa wakazi  hao hakutaka jina lake  litajwe  amesema kuwa kutokana na ukuaji wa mji Dodoma utakuwa na ukuaji wa kilometa 50 hivyo ameshauri  dampo hilo lingesogezwa liwe kilometa 60 liwe mbali na mjini

Kutokana na Ongezeko la watu nchini kwa miji mikubwa inaongezeka kwa kasi ukichukulia jiji la Dar es salaam ndani ya miaka 10 ongezeko limekuwa kubwa hivyo kwa mji  Dodoma unatakiwa kupangwa kwa miaka mingi ijayo ili kwamba usilete mabadiliko katika kipindi kifupi.


No comments