KUELEKEA MKUTANO MKUU WA 5 MVIWATA.


Mwenyekiti wa mviwata Mkoa WA Arusha bwana Richard kipara akisoma taarifa katika mkutano wa mtandao wa vikundi vya wakulima Mviwata Mkoani Arusha.

Baadhi ya wanachama wa mviwata

ARUSHA

Mtandao wa vikundi vya wakulima Nchini Tanzania(MVIWATA) umeendelea kutoa elimu juu ya matumizi chanya ya viatilifu katika sekta ya kilimo na ufugaji ikiwa ni sehemu ya udhibiti wa ubora wa viatilifu hivyo kwa maslahi ya afya ya mlaji pamoja na mkulima ili kuweza kuleta maendeleo kwa taifa.

Wakizungumza katika mkutano Maalumu uliowakutanisha wakulima na wafugaji kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini mwenyekiti wa mtandao huo Mkoani Arusha Bw Richard Kipara

amesema kwamba ni muhimu kuboresha uzalishaji, masoko na uhifadhi mazingira kwa Kilimo endelevu na kuachana na Kilimo cha mazoea.

Kwa upande wake Gaspar Urio ambae ni bwana shamba akatumia fursa hiyo kusisitiza matumizi sahihi ya viatilifu katika uzalishaji bora wa mazao ya chakula na biashara pamoja na umakini kwa wafanya biashara wa viatilifu

Aidha nao baadhi ya wakulima na wafungaji waliopata fursa ya kushiriki mkutano huo wa Masuala ya Kilimo wakaeleza matarajio yao katika Kilimo chenye tija, Ambapo pia wamesema wataalamu waendelee kutoa elimu kuhusu Kilimo bora na matumizi sahihi ya viatilifu.

Kauli mbiu ya mkutano huo Mkuu wa tano wa Masuala ya kilimo na ufugaji ni "Dhibiti wa ubora wa viatilifu kwa afya ya walaji na maslahi ya wakulima".


                             




No comments