MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI TIRA KANDA YA KASKAZINI YATOA ANGALIZO

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Adelaida Muganyizi akitoa ufafanuzi wa jambo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipotembelea katika banda hilo katika maonyesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika Kitaifa mkoani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza (aliyevaa miwani) akimsililiza kwa makini mmoja wa Askari polisi aliyetembelea banda hilo kwaajili ya kupata elimu zaidi kuhusiana na Bima.Picha na Vero Ignatus Blog.
Afisa Sheria mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Kaskazini Okoka Mgavilenzi (wa kwanza kushoto ) akiwa anamsisitizia jambo mgeni aliyetembelea banda hilo,akifuaatiwa na Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza

TIRA wakiendelea kutoa elimu ya Bima kwa wageni mbalimbali waliotembelea banda hilo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus,Moshi -Kilimanjaro
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini( TIRA) imetaka Jamii kufahamu umuhimu wa bima ili kwamba anapokumbana na janga lolote waweze kupata stahiki zao kwa mujibu wa sheria namba 10 ya bima ya mwaka 2009 kwani chombo hicho kimeundwa kwaajili ya maslahi ya mlaji (watumiaji wa bima)
Mkurugenzi wa masoko na utafiti (TIRA ) Bi. Adelaida Muganyizi amesema kuwa lengo kuu la wao kuwepo katika maonyesho ya wiki ya nenda kwa usalama baranarani Moshi Kilimanjaro ni kutoa elimu kwa jamii ili kufahamu vyema faida za huduma ya bima,mikataba ya bima ,wafahamu umuhimu wa kuwa na bima na kuzitambua haki zao huku kujua kuwa panapo haki pana wajibu.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Bima Eliezer Rweikiza amewaagiza mameneja wote na wale wote wanaotoa huduma, kufuata sheria za bima, kutoa huduma kwa wananchi inayokidhi mahitaji yao ili kuleta mrejesho katika jamii kwa wale waliopewa huduma ya bima uwe chanya na huduma hiyo watu wengi waweze kuifikia .
Ametoa agizo kwa wale wote wanaotoa huduma hizo haswa kwa vyombo vya moto, wahakikishe taarifa zote zimeingia kwenye mfumo ambao mamlaka imeubuni kwaajili ya kufanya tathimini mbalimbali katika kuendeleza soko na huduma za bima,amewataka pia wananchi kukata bima kwaajili ya mali zao,afya,wakate bima kwaajili ya kitu chochochote walichonacho ikiwepo Elimu ili waweze kujikinga na majanga yanayoweza kuwapata wakati wakiwa hawana uwezo wa kuamka wenyewe.
Rweikiza amesema Mamlaka hiyo inajukumu la kusimamia shughuli zote kuanzia shughuli za usajili wa makampuni,madalali ,malalamiko pamoja na wakala na kuangalia utendaji wa soko katika kanda na kuhakikisha unafuata sheria ya bima na wanafanya ukaguzi ili kufahamu utendaji wa watoa huduma za bima kama wanafuata taratibu zote kwa vigezo ambavyo vimewekwa ili wavifuate.
Kwa uande wake Afisa Sheria mwandamizi wa mamlaka hiyo ya Bima Okoka Jailo Mavilenzi amesema kuwa kifungu cha sheria (61) kinamtaka kila mtu anayejishughulisha na shughuli za bima haswa za vyombo vya moto inamtaka kuhakikisha kuwa anakata bima kwenye makampuni yaliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 10 ya mwaka 2009 ya usimamizi wa bima .
Amesisitiza kwamba kuwakatia watu bima ambayo siyo halali ni kosa kisheria ,Kwani Sheria ya bima katika kifungu (161)kinasema ni kosa kwa mtu yeyote kufanya biashara ya bima akiwa hajasajiliwa mtu huyo akikakamatwa anafikishwa polisi ushahidi unapokamilika anapelekwa mahakamani,akipatikana na hatia kwa kosa hilo sheria inasema atatozwa faini isiyopungua milioni tano au kifungo cha miaka miwili jela au adhabu zote kwa pamoja .
Sambamba na hayo Mamlaka hiyo imekuja na mfumo wa kuhakiki stika za bima ili waweze kukabiliana na tatizo la stika feki ambapo amesema kuwa mtu anapojihusisha na kughushi nyaraka zozote zile zikiwemo nyaraka za bima kama vile stika anafanya kosa chini ya kifungu cha sheria namba 336,335 na 337 cha kanuni ya adhabu ya 16 marejeo ya mwaka 2002, ambapo mtu akipatikana na hatia kwa kosa hilo la kughushi sheria inasema anatakiwa kufungwa kwa miaka isiyozidi miaka 7



No comments