Makamu wa Rais Kuzindua wiki Nenda kwa Usalama Barabarani Kilimanjaro Leo.

Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshawasili mkoani Kilimanjaro  jana na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro,  Anna Mghwira pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Makamu wa rais anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Kilimanjaro.

Maadhimisho hayo yatafanyika leo Jumatatu katika viwanja vya Mashujaa Moshi ikiwa na kauli mbiu isemayo "Zuia ajali tii sheria okoa maisha.

No comments