MAKAMU WA RAIS AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOANI KILIMANJARO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Koplo Faustina Ndunguru kutoka Makao Makuu ya Trafiki kitengo cha Elimu ya Usalama Barabarani katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira (kushoto) na Kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Usalama na Mazingira kutoka TANROADS Makao Makuu Bi. Zafarani Madayi wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho yanayotoa elimu ya usalama barabarani katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Msaidizi Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Joyce Mbunju akimuelezea Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan namna Wizara ilivyojipanga nakuja na mbinu za teknolojia ya kisasa katika kuhakikisha usalama barabarani unakuwepo wakati wote.
Mwanafunzi wa Darasa la 5 kutoka shule ya msingi Muungano Bi. Aisha Ayoub akishiriki kuima nyimbo za kuelimisha masuala ya usalama barabarani akiwa mmoja kati ya wanafunzi waliotoka shule 10 za Manispaa ya Moshi mjini wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambao umefanyika katika viwanja vya Mashujaa ambapo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.
Makamu wa Rais Samia Suluhu amezindua rasmi wiki ya nenda kwa usalama barabarani inayofanyika litaifa mkoani Kilimanjaro yenye kauli mbiu isemayo "Zuia ajali -Tii sheria -okoa maisha."
Jumla ya ajali 125 zinatokea kwa mwaka duniani , amesema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuona Tanzania inatajwa katika ripoti ya Shirika la Afya duniani kuwa ni nchi inayoongoza kwa ajali duniani ikiwa na asilimia 32.9 na wanaopoteza maisha ni vijana walio kati ya umri wa miaka 18 - 29 sawa na asilimia 74 wengi wao wakiwa ni wanaume.
"Kama sisi tunachangia asilimia 32.9 basi muda sasa wa sisi kama nchi kujitathmini ,asilimia hizi zinaashiria kuwa ajali zinasababisha vifo vingi kuliko magonjwa"alisema
Amesema 76% ajali husababishwa na makosa ya kibinadamu kama vile uchovu wa madereva,utumiaji wa simu wakati wa kuendesha na ulevi wakati mwingine hisababishwa na hali mbaya ya barabara 8% ubovu wa magari au matatizo ya kiufundi 16%
Kuanzia Januari -Septemba katika mikoabya Tanzania Bara kumekuwa na ajali 4,2721 zimeua watu 1,613 na kusababisha majeruhi 1,597 kati ya hizi mkoa wa Kilimanjaro uliripotiwa kuwa na ajali za 84 za pikipiki vifo 61 na majeruhi 21 ajali hizi nyingi zimewaacha wengi wakiwa walemavu wa kudumu.
Amelitaka Baraza la Usalama Nchini kufanya kazi ya kuhamasisha ummaa juu ya hatari iliyopo barabarani na mikakati huo uwafikie viongozj mbalimbali kuanzia ngazi ya Mkoa,Wilaya,Tarafa na hata vijijini ili wananchi waelimike zaidi juu ya hatari za usalama barabarani zinazowakabili katika zama hizi za ongezeko kubwa la vyombo vya usafiri.

No comments